Majuma kadhaa yaliyopita, yule mshambuliaji wa kujitoa Mhanga aitwae Hussein Bashe (Certificate CBE) alitoa tuhumua nzito dhidi ya Waziri Membe, akimhusisha na tukio baya la shambulio dhidi ya Mhariri nguli wa magazeti ya New Habari Corportion, mmoja Bwana Absalom Kibanda ambaye bado anahudhuria matibabu huko Afrika Kusini. Huku wenye akili zetu tukijua na kuamini kwamba tuhuma zile zilichochewa na chuki dhidi ya mtuhumiwa na mchezo wa kisiasa uliopangiliwa vilivyo na mafisadi wasioisha kuweweseka, juma moja lililopita mwanasiasa na wakili mahiri nchini Mabere Marando alikuja na tuhuma na majina kumi ya watu ambao kwa madai yake ndiyo waliohusika na ukatili huo na ule aliofanyiwa Dr. Steven Ulimboka. Katika majina hayo, ambayo mtoa tuhuma alisema ana ushahidi wa kuhusika kwao, jina la Membe halikutajwa wala kuhusiahwa na unyama huu.
Hili bila shaka ni pigo kwa mshambuliaji huyu (Bashe) na principals wake maana sasa umma wa watanzania umebaini kwamba madai ya Bashe yalichochewa na chuki na kujihami, kwa staili ile ile ya Dodoma. Hakika Bashe amejivika kilemba cha kichekesho na kulazimika kuula mkate wa majonzi!