The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Wanajamii habari zenu?
Baada ya kukaa na mpenzi huyu ambaye sasa kila kukicha naonja joto la jiwe, sasa nimeanza kumkumbuka mpenzi wangu wa zamani ambaye alinijali kwa hali zote, alinikuta nikiwa sina lolote lakini alinipenda toka ndani ya moyo wake.
Nakumbuka kuna kipindi nilijisikia kumchukia tu bila sababu. Nikawa nasababisha ugomvi kila mara. Na mara zote ni yeye aliyeniomba msamaha ingawa ni mimi niliyesababisha kutoelewana.
Kuna siku nakumbuka nilikuwa kwenye matatizo ya kikazi, ni yeye aliyesimamia kila kitu kuanzia kula yangu mpaka madeni yangu. Baada ya kumaliza shida zangu na kurudi kazini, nilimpigia simu na kumwambia nilikuwa namtumia tu na wala simpendi. Muda huo sikujisikia vibaya. Ila leo najutia kwa kitendo hicho.
Natamani nirudi mikononi mwake na kutulia maisha yangu yote kutokana na upendo na kujali kupindukia.
Mungu anisamehe kwa kumuumiza sana.