Natamani kumwandikia Waziri/Rais barua pepe

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,934
5,037
Nilikuwa na angalia website za Nchi zilizo endelea kama marekani nikaona mtu wa kawaida anaweza kumuandikia barua/email waziri au Raisi direct (Moja kwa moja bila kupitia kwa wapambe wengi wanaoweza kuchuja hata mambo mazuri)
Kinacho takiwa ni email fupi ya maneno yasiyo zidi idadi flani (300?) ili wasijaze nafasi

Ule ukurasa utakulazimisha ujaze taarifa zako za kweli
  1. Jina kamili
  2. Kitambulisho cha kura/passport
  3. Namba ya simu & email
  4. mahali unapoishi
  5. Nyumba # au Mtaa

Mimi niliona kama ni fursa kwa watu wenye nia njema na waziri/Raisi kwani hao viongozi wakuu watapata fursa ya moja kwa moja kuwasiliana na wapiga kura na pengine kupata mawazo muhimu yanayo weza kurahisisha utendaji wao

Natamani na hapa kwetu tuwe na hiyo fursa
 
Mpiga kura wa kagera nkanda, kasulu vijijini, kigoma, Tanzania anawezaje kutuma email?
 
Nikupe namba zake hata akibadilisha leo nakuwa nayo!!
Ila usijisumbue utaishia kubambikiwa mikesi acha na tamaa weka pembeni unafiki subiri mungu ndio hutoa kwa wakati wake hivyo vyeo!!!
 
Naunga mkono Vampire
hakuwezi kuwa na mfumo utakaonufaisha kila mmoja as an individual....Na si lazima kila raia aweze kutumia...Ni kama teknolojia yoyote duniani, zina manufaa makubwa lakini si kuwa kila mtu katika dunia hii anazitumia

Pia ikumbukwe kuwa; kuandika sio kwa ajili ya kumsalimia muheshiwa; ni pale tu kutakapo kuwa na hoja ya msingi na MUHIMU.
 
Nilikuwa na angalia website za Nchi zilizo endelea kama marekani nikaona mtu wa kawaida anaweza kumuandikia barua/email waziri au Raisi direct (Moja kwa moja bila kupitia kwa wapambe wengi wanaoweza kuchuja hata mambo mazuri)
Kinacho takiwa ni email fupi ya maneno yasiyo zidi idadi flani (300?) ili wasijaze nafasi

Ule ukurasa utakulazimisha ujaze taarifa zako za kweli
  1. Jina kamili
  2. Kitambulisho cha kura/passport
  3. Namba ya simu & email
  4. mahali unapoishi
  5. Nyumba # au Mtaa

Mimi niliona kama ni fursa kwa watu wenye nia njema na waziri/Raisi kwani hao viongozi wakuu watapata fursa ya moja kwa moja kuwasiliana na wapiga kura na pengine kupata mawazo muhimu yanayo weza kurahisisha utendaji wao

Natamani na hapa kwetu tuwe na hiyo fursa
We andika hapahapa ataiona, tena utasaidiwa kuuboresha ujumbe wako kama haukidhi haja!
 
Back
Top Bottom