Natamani kikosi cha Simba kesho kiwe hivi

jaykiwele

JF-Expert Member
May 22, 2013
553
500
Hiki ndio kikosi nataman kianze kesho kwenye mechi ya kombe la klabu bingwa baran afrika Kati ya Simba na Al ahly. Kwanza napenda kusema kwamba sina lengo la kumpinga kocha au kumpangia majukumu kocha mkuu wa Simba Bw. Patrick Aussems ila Kama mdau na shabiki kindaki ndaki wa Simba na kutokan nimefuatilia kikosi Cha Simba tangu msimu huu uanze ningetaman kikosi kiwe hivi:-
1. Aishi Manula
- huyu ndio kipa namba moja kwasasa japokuwa amekuwa na makosa mengi hivi karibun lakin kwa uzoefu na uhodari wake bado unamweka juu kuliko makipa wenzake.

2. Gyan
- huyu ni mzuri zaidi kwa mechi hii maana hii mechi ni ya kushambulia zaidi hivyo uwepo wake utasaidia kupeleka mashambuliz ya haraka upande wa kulia na kupeleka kilio kwa waarabu japo baadae anaweza kutolewa na kuingizwa mchezaj mwingine wa kusaidia ulinz maana Gyan ana makosa mengi kweny kujilinda.

3. Mohamed Hussein (shabalala)
- amekuwa kweny kiwango kizur na ameimarika zaidi kupandisha team kushambulia tofaut na kwasi ambaye hajapat match fitness ya kutosha

4. Erasto Nyoni ( Kama kapona)
- Taarifa zinaonesha jamaa amerud japo team bado haijaweka wazi ila Kama kwel karud aanze tu huyu ni chuma cha maana anafany kazi kubwa sana hasa kuituliza team pale nyuma ila Kama bado acheze tu juuko japo simkubali Sana maana ana papara sana juuko.

5. Serge Wawa
- ana mapunguf mengi ila ndio mchezaj mzoefu zaidi wa kimataifa kweny kikosi nadhan akijirekebisha anaweza kuwa msaada sana kwa team hasa kuanzisha mashambuliz ya haraka.

6 James Kotei
- Huyu ndio nguzo kuu ya team kazi kubwa anayofany pale katikat hakuwa asiyeiona na Mara zote akipotea basi tunapata shida Sana ila nategemea atakuwa kwenye kiwango chake hivyo kutimiza majukumu yake ya kutibua mipango ya wapinzan na kuanzisha mashambuliz akishirikian na wenzake pale katikat.

7. Jonas mkude
- wenyew tunamuita mtoto wa msimbazi ni moja ya kati ya wachezaj wenye uchungu Sana kweny team na Mara zote amekuwa mwamba anayeweza kutawala pale katikat na uwezo mkubwa kumilikk mpira hivyo kusaidia kupeleka mashambuliz kwa Al ahly na kuwatuliza

8. Clatous chama
- huyu ndio Mastermind wa team anapanga mipango yote ya mashambuliz na pia anaweza kufunga kwa ustadi hakuna Shaka juu kuanza kwake.

9. John Boko
- Boko anauwezo mkubwa wa kuwasumbua mabeki wa Kati wa Al ahly na kutokan na mwili wake itapelekea kuwachosha mabeki hivyo kuwapa nafas kuwaangamiza kabisa waarabu hawa Wala ngamia

10. Emmanuel Okwi
- huyu ndio muuaji pekee wa waarabu hakuna mwenye swali juu ya hilo bahat nzuri kule misri hakuonesha makali yake hivyo watakuja kwa kumdharau ila atakuwa muuaji kesho

11. Haruna Niyonzima
- wengi watashangaa kwanini haruna sio medie kagere au mzamiru? jibu pekee hapo ni kwamba huyu fundi anatakiwa aanze ili nguvu ya mashambuliz iwe kubwa maana Al ahly hawamfaham vizur huyu mtoto wa Rwanda na akiwa kwenye kiwango chake anaweza kuwa msumari wa Moto atakayeongoza kuwaua waarabu pale kwa mchina. Kesho hatuhitaj kusubiri Sana kuwaua hawa jamaa mapema tu wapigwe waanze kuwaza kurudi kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom