sbikore
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 535
- 191
Habari zenu wana ndugu!!
Ni muda mrefu sana nimekuwa nayavumilia mambo ya kipuuz yaliyoendea kusemwa dhidi ya kiongozi wangu Mh.rais,lakin sasa nimeamua kutoka hadharani kiyakemea na ikiwezekana kuzishawishi sehemu husika kupambana na udhalimu huu.
Ni juzi tu uchaguzi umemalizika na tulichotegemea watanzania wote ni kumuunga mkono rais wetu kuyashushulikia matatizo ya watanzania hasa wanyonge kwa kiwango cha juu na kama alivyoahidi yy mwenyewe.
Kwa uaminifu wake mkubwa aliopewa na mungu ameendelea kutembea katika maneno yake aliyoyanadi pindi anaomba kura,na huu ndio ulikuwa msingi wa utawala wake c tu kwa kuurithi kutoka CCM,bali hata kwa vyama vingine na hasa CHADEMA.
Lakini tunashangaa kadri anavyozidi kusonga wapo wapuuz wanamshika miguu kwa maksudi tu kwa kulinda nafasi zao za kisiasa. Nchi hii ina mihimili mikuu mitatu ambayo ni;Bunge,Mahakama na Serikali.Mihimili yote hii inafanya kazi bila kuingiliwa na mhimili mwingine.
Sasa cha kushangaza kila mhimili unapotekeleza wajibu wake wa kazi hautizamwi na badala yake anatajwa raisi bila kujua kwamba kila mhimili kati ya hiyo unazo taritibu na misingi uliojiwekea kwa ajili ya kifanikisha majukimu yake ya kila cku.
Na ikumbukwe rais yako matamko anaweza yatoa wakati na mahali popote kwa mamlaka aliyopewa na katiba/sheria mama ya nchi kama vile majipu anayoyatumbua. Ametoa matamko mengi ya utumbuaji lakini cha ajabu hawahawa wapinzani waliojiita watetea haki za wanyoge waliibuka kupambana dhidi ya shughuli ngumu anayoikamilisha rais.Wamekuwa mstari wa mbele kwa kuja na hoja changa kwamba haki za binadamu.
Hiyo tu haitoshi;Mahakama imemhukumu mtu aliyemtusi rais mtandaoni,wametoka na motivation ya kumchangia ili asifungwe,tena zoezi hili linaendeshwa na wanasisa bila hata aibu. Kwa maana hiyo wanawafudisha wananchi ujinga wa kuligeuza kosa kuwa halali,tena wakitambua huyu ni kiongozi wa mwisho wa nchi. Bungeni wamekiuka wenyewe kanuni za bunge,zimewatema nje,matokeo wanasema rais anabana demokrasia.
Sasa wamekimbilia mtaani nako wamepambana na majeshi ya kulinda usalama,kwa kusimamia taratibu za kazi jeshi la polisi limetoa amri ya kusitiswa mikutano na maandamano nchi nzima bila kujali vyama. Kwa kiburi tu wapinzani wameendesha mikutano kahama na sehemu nyingine za nchi,polisi imechukua hatua lakini lawama kabeba mh.rais.
Naamini mti wenye matunda mema hupondwa mawe.Rais Magufuli ametekeleza vyema wajibu wake ndio maana sasa hata akiharibu flani basi anaitwa Magufuli,hii yoote ni baada ya kuona wanazidi kuzikwa kisiasa,wanaanzisha harakati za hovyohovyo,harakati za kichochezi na zinapokelewa na wajinga flani tu waliozoea kulalamika maisha yao yoote bila hata sababu za msingi.
Lakini ikumbukwe kuwa harakati hizi dhalimu muda woote zinaendeshwa,Mh.rais yuko kimya kabisa na anatekekeleza majukumu ya kitaifa ya kila cku na bila hata kutaja majina ya wanasiasa hawa wanaomchafua. Sasa naamini saa imewadiwa Mh.rais awatumbue hawa wachache wasiolitakia mema taifa hili.Maana naamini harakati zao hizi za kijinga ikitokea zikazua machafuko bado yy kama baba mwenye nyumba atazibeba lawama.
Nakuomba mh.rais wangu kuanza kuchukua hatua kwa hawa;
Mbowe,Zitto pamoja na wafuasi wao.Na ikiwezekana kuwepo utaratibu wa kuwaelekeza kila mbunge akafanye harakati hizi uchwara ndani ya jimbo lake na sii hivi wanavyofanya.
Naomba niwasilishe.