Udhaifu wa hayo ya zamani ndo umefanya tukimbilie mapya... hasahasa ujambazi wa Tigo na vodaKwanini mnakurupuka na makampuni mapya? Au walikuwa wanagawa lunch na dinner bure? Hata miez miwili hauna tayari mtu ashatimkia huko....hahah isomeni tu namba, tunalipa madeni ya uchaguzi
Kuna tofauti kati ya spidi bila kikomo na internet bila kikomo, wewe umepewa spidi kubwa zaidi isiyokata kata Ina maana uki download application zenye ukubwa wa mb hizo kwisho habari yako.Kwa kuwa hii tabia ya makampuni ya simu kutuibia kwa kufanya ulaghai imezidi huku mamlaka husika zikiwa kimya kama hazina kazi (TCRA ni jipu watumbuliwe tuu maana hakuna namna ) sasa naamini ni muda muafaka wa kampuni moja kuonyeshwa mfano..
Nianze na hawa halotel ambao wanasifika kwa mtandao mzuri na kweli wana net ya ukweli, wana bundle lao ambalo wanaliita la spidi bila kikomo(800mb kwa buku), nadhani watu wote tunaelewa maana ya neno bila kikomo..
Nimenunua hili Bundle nikadownload kama application 2 wakantumia message kuwa kwamba nimefika kiwango cha mwisho cha spidi hivyo .. yaani application 2 tu... nikaanza kujiuliza maana ya neno spidi bila kikomo ni nini na kwanini walisema ni spidi bila kikomo. najaribu kufikiria wakifanyia watu 100000 kila siku kama hivyo wanapata bei gani kwa ulaghai huu..
Hapo sijataja wizi wa vocha umeweka unakuta imekatwa wamekuunga wenyewe na huduma wanazo jua wao (kama Tigo ndo maexpert wa hii kitu)...
Nimekuja kupata hitimisho kuwa haya makampuni yote ya simu yapo kifaida zaidi kiasi kwamba hawajali kabisa huduma wanazotoa..
Hakuna wa afadhali ila ntaanza na nyie halotel maana mmekuja juzijuzi tuu mshaanza kujifunza umafia , mkifikisha miaka 10 si mtaua watu.
Boss nafahamu tofauti ya unlimited speed na unlimited data..Kuna tofauti kati ya spidi bila kikomo na internet bila kikomo, wewe umepewa spidi kubwa zaidi isiyokata kata Ina maana uki download application zenye ukubwa wa mb hizo kwisho habari yako.
Na Internet bila kikomo ni wanakupa internet access kwa makubaliano ya siku, wiki au mwezi bila kukata hapo kidogo nadhani umeelewa na nakushauri watafute wanasheria wakutafsrie hiyo kauli kabla ya kuwashtaki maana usije ukawa walipa
ndugu yangu hao tcra wakisikia fulani kamtukana kiongozi an kumsimanga watafanya chini juu wakukamate, kwa hili utangoja sanahili tulishalijua mapema, wapo wengi wanalizwa ila wanakosa pakusemea..
Kibaya zaidi hata TCRA wanalijua hilo, lakini wanalifumbia macho.