Nataka nikasomee Sheria pale UDSM, naomba ushauri

MBUNIFUmdogo

Member
Oct 15, 2015
40
9
Habari wanajamvi, kwa kuanzia na point ni kwamba,nataka kwenda kusoma digrii ya sheria (law) pale UDSM.

Vipi kuhusu soko lake?
 
Je,unaipenda sheria kutoka moyoni?
Soko lake ni akili yako,jinsi utakavyojipambanua mwenyewe na kuwavutia wateja.
 
Soko lipo, kama uelewa wako utameet market demands....jipange tu vizuri maana udsl si lele mama!
 
Katika Maisha yako yote usikae ujaribu kusomea kitu eti kwasababu ya kuangalia soko..somea kitu unachokipenda kutoka moyoni.
Watakwambia hapa sheria ni nzuri,baada ya kuanza utakutana na mtu atakwambia wanasheria wako wengi..utakata tamaa utaishia kupata vi-GPA vya 2.6 ndo umepasua!!
 
ukisha maliza unataka kuwa nani? maana kabla sijachangia kitu nijue maana watu kama ww wakimaliza taaluma kama hiyo wanawafukuza wenzao BUNGENI
 
Kwa sasa sikushauri sana. Kwanza sheria ni ngumu sana kuisomea. Utasota na makabrasha. Pili inachukua miaka mingi. Maana ukimaliza utatakiwa kwenda law school na ku practice pia itachukua muda. Tatu soko la ajira nalo liko saturated so itakuwa tait kupata ajira (japo kila mtu na bahati yake)...
 
Kama ni form 6 leaver subiri tokeo litoke kwanza.. Then mambo mengine yatafuata
 
Kama ni form 6 leaver subiri tokeo litoke kwanza.. Then mambo mengine yatafuata

Ni vizuri ukianza kufikiri sasa majibu yakitoka unakamilisha na ku-apply otherwise utakuwa under pressure. Sasa hivi unaweza kuangalia vyuo vipi vinatoa hiyo program na zinatofauti gani etc.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom