Nataka NAPE ujibu hili

Nataka NAPE ujibu hili

Jamani huo ndio uenezi wenyewe,unadhani akiri mojakwamoja
 
Nape ni mhimu kulaini vitendo kama hivo badala ya kulinda heshima ya chama

Huwezi kulinda heshima ya chama kwa kusema uongo; kama mjeruhiwa anawafahamu kwa majina na sura, gari lilikuwepo hapo hadi polisi wamefika, je Nape anauhakika gani kuwa anaowasema MBUNGE sio wenyewe hivyo sio sahihi?? basi anawajua vizuri na aisaidie polisi kuwakamata. Ukweli ni kwamba mapanga hubebwa na watu, na kila mtu anaweza kubeba hayo mapanga; Hivyo ni vema kuacha na kukemea mbinu za kishenzi kama hizo.
 
Nape hakutakiwa kukiri wala kukana kuhusika kwa wanachama wa CCM. Mhalifu anaweza kuwa wa chama chochote, cha msingi upelelezi wa haraka na wa kina ufanyike na wakibainika ni wafuasi wa ccm basi anaweza kusema sasa kwamba "hata hivyo chama hakikuwatuma"

Kukanusha moja kwa moja kunaonyesha anajua kitu.
 
Nape siku hizi umekuwaje ndugu yangu? kuna kipindi nilikuwa nakuona shujaa balaa!
hasa kipindi kile Lowasa alipoingiza ufisadi kwenye lile jengo la vijana pale Lumumba!
sasa hivi umekuwa mtu wa ajabu sana!

Mkuu kipindi hicho hakuwa na cheo. Na hii ndo tofauti ya CCM na CDM. CCM mtu akita cheo tu, utu maadili na busara zake zinapumzika.(SITA na Mwakembe wamepewa uwaziri wamekuwa vinyonga wanabadirika rangi kila kukicha) wakati CDM cheo huchochea kasi ya ubunifu na uchapakazi.
 
Back
Top Bottom