Nataka Mama yangu akistaafu kazi nioe

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,612
21,346
Jamani habari za uko? bila shaka ni njema.
Leo nataka niwashirikishe habari njema ambayo imekuwa ikizunguka kichwani mwangu kwa muda wa wiki kadhaa,

Kwanza kabisa mimi ni kijana wa miaka 37 sijafanikiwa kuajiriwa, kwa hiyo mara nyingi huwa nasaidia saidia kazi za hapa nyumbani. Wiki hii nimejifikiria sana kuhusu suala la kuoa na hivyo kupata wazo la kuchukua hela kidogo ya pensheni ya mama, maana atastafu muda si mrefu ili niende kuolea maana kuoa siku hizi ni gharama halafu mimi sina kazi, nadhani nitatumia kama asilimia 50 ya pensheni ya mother.

Ombi langu kutoka kwenu wanaJF ni kutaka ushauri nioe wanawake wa aina gani wasio na makuu pia wale ambao mmeoa naombeni mnipe tips kidogo. Maana sharing is caring
 
Kisa cha kutokuwa na kazi ni nini?
au hupendi kufanya kazi?
ujue kuwa na mke nayo ni kazi, sasaaaa.......sijui

pensheni usiifikirie kwa sababu ni jasho la mtu mwingine, nje ya hapo unatafuta laana maana akikunyima unaweza hata kumfanyia ubaya.....e.g. kumwibia, kumuua n.k

samahani saaana kama nimekukwaza
 
Duh! Kutumia asilimia hamsini ya pension ya mama ako, hiyo pension analipwa ni sh miloni mbili nini? Infact kuoa ni jambo jema. Ila angalia lisikugharimu sana...
 
Tobaaaaaaaaaaaa mungu tunusuru,yani ivi una 37 au 27? huna mtoto hata wakusingiziwa mpaka sasa? kama una 37 sasa mpaka uoe ujipinde sana huyo mtoto ukimpata una 40, sasa Mama amekusomesha na bado anakulisha mpaka sasa
unabahati wewe kaka zangu wanaona wakiwa chuo mke anakaa nyumbani kwetu mpaka wakimaliza wana watoto kama si 1 wa2 halafu anaanza kazi anachukua familia yake,sasaivi wa 37 yrs ana 6kids na amesha maliza analea watoto wake
wewe ndio kwanzaaaa unachuria pesa ya MAMA,wewe mwanamme wawapi sio wa DAR?
 
jesus christ!! 37 years with this kind of crap idea??? wonders shall never end....uolee kiinua mgongo cha mzaz wako ulete njaa nyumbani..kweli wewe hamna kitu ni zero brain blali faucken...huna akili ya maisha wala ya kazi.....kufa
 
Jaman wanaume wa kweli tunazidi kupingua, miaka 37 anaamka asubuhu anaomba ela ya vitafunwa na ya wembe akanyolee alafu anaiwazia pensheni ya bi mkubwa aoleee then mke ampeleke kwa bi mkubwa
 
Mwanaume Miaka 37 huna shughuli inayokuingizia kipato? Am sorry to say this: wewe ni mwanaume mzembe tena level phd. Ulitakiwa uwe wa kwanza kumsapoti mama yako financially badala yake unataka kutumia kiinua mgongo cha mama ili uoe. Nilidhani ht ungesema ushirikiane na mama kufanya mradi na hiyo pesa.
Nahisi hata ukishaoa hiyo 50% iliyobakia utaichukua utumie kutunza familia yako. Huyo mke mtarajiwa namuonea huruma maana kapata bonge la zigo. Unatia aibu wanaume wenzako.
 
Mkuu mwachie mama yako penshen yake haikuhusu bd yuko hai
Km unataka kuoa tafta mwanamke level yako uoe kuna baadhi ya wanawake wanauhitaj sana wa kuolewa hata mahar anaweza akupe upeleke kwao
 
Back
Top Bottom