Nataka kuwa Mtafiti (Researcher)

small mind

Senior Member
Jun 1, 2012
129
58
Habari za wakti huu,

Mimi ni mwanaume 30+ Nahitaji kujiingiza katika fani ya Utafiti (Bado sijachagua eneo la uzamifu) Ingawa napendelea zaidi kuwa mtafiti katika eneo la Sayansi ya Jamii ambalo naamini ni eneo ambalo bado linahitaji tafiti za kina katika mambo anuai.

Ombi langu kwa sasa ni kutaka kupata ushauri kutoka kwa wana JF kuhusu shughuli za utafiti kama biashara, huduma je zinalipa? Je fursa zipo za kutosha? Je ni kwa namna naweza kuanzisha shughuli za utafiti kwa hapa Tanzania?

Asanteni
 
Ukiwa mtafiti wa masoko (marketing research)
Nadhani itakulipa zaidi.
Japokuwa Mimi si mjuzi wa mambo hayo
 
Ni biashara nzuri inayoweza kukuingizia kipato kikubwa kwa haraka kama una uwezo mkubwa wa kuandika proposal na ripoti. Pia uwe na uzoefu kwenye utafiti, kwani wakati mwingine ukijibu T.O.R wanakuambia uambatanishe sample ya kazi ulizofanya.

Wateja wakubwa ni mashirika yasiyo ya kiserikali kama USAID, GIZ, WORLD VISION, WFP n.k

Zaidi ya miaka 10 nimekuwa kwenye hii fani, nilifanya kwenye shirika moja kwa miaka 5, sasa hivi nafanya kama freelancer (mtafiti wa kujitegemea).

Jitahidi uwe vizuri kwenye software kama;
Excel especially upande wa Pivoting
R ,Python, SPSS kwa ajili ya data analysis.
Kama unaweza jifunze ODK (open data kit) inatumika kuprogram maswali na kukusanya data kwenye simu janja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
T.O.R? naomba ufafanuzi

TOR ni Terms of Reference, kwa kiswahili chepesi ni tangazo ambalo mwombaji anatakiwa kujibu. TOR inatoa mwongozo kwa mwombaji kuhusu mradi na nini kinatakiwa kifanyike kwenye hiyo kazi. nimeabatanisha mfano wa TOR upate mwanga zaidi.
 
Attachments

  • TOR-KNK-Baseline-survey.pdf
    152.3 KB · Views: 9
Ni biashara nzuri inayoweza kukuingizia kipato kikubwa kwa haraka kama una uwezo mkubwa wa kuandika proposal na ripoti. Pia uwe na uzoefu kwenye utafiti, kwani wakati mwingine ukijibu T.O.R wanakuambia uambatanishe sample ya kazi ulizofanya.

Wateja wakubwa ni mashirika yasiyo ya kiserikali kama USAID, GIZ, WORLD VISION, WFP n.k

Zaidi ya miaka 10 nimekuwa kwenye hii fani, nilifanya kwenye shirika moja kwa miaka 5, sasa hivi nafanya kama freelancer (mtafiti wa kujitegemea).

Jitahidi uwe vizuri kwenye software kama;
Excel especially upande wa Pivoting
R ,Python, SPSS kwa ajili ya data analysis.
Kama unaweza jifunze ODK (open data kit) inatumika kuprogram maswali na kukusanya data kwenye simu janja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Good
Naomna nijifunze kwako kuwa mtafiti freelancer mkuu
Ntaku pm
 
Je una sifa za kuwa mtafiti? Kazi nyingi za utafiti zinahitaji kuwa na shahada za uzamivu katika fani unayoitafiti. Otherwise utakuwa data collector/ mtafiti msaidizi.
 
Back
Top Bottom