Ngahekapahi
JF-Expert Member
- May 8, 2012
- 553
- 371
Mkuu chukua ipad 4 or ipad Air hutajuta.
Portable wifi router ya chni kabisa bei gan? na msaada matumiz yake ni mshamba kdogo hapo nlitaka kununua..
Namie pia ningependa kujua bei za hiza WIFI router kwa hapa bongo ukizingatia kuna uwezekano wa kusave pesa kidogo kwa kununua WIFI TAB badala ya 3G/4G tab ambazo ziko juu kdogo
Bei za Portable WiFi Router (zenye betri ambazo unachaji) zinatofautiana, threads zake zimo humu jf, tafuta usome. Mimi napendelea products za kampuni ya Apple, ila hii thread ilinisaidia sana sababu sikuwa najuwa kama kuna Tablets ambazo hazitumii Sim card. Ushauri wangu kwako, nunua Tablet yenye kutumia Sim Card sababu unaweza ukatumia kama Simu pale inapohitajika.
Nilinunua WiFi Router kwa ajili ya kupunguza gharama za kujiunga na bundles kwa kila kifaa nachotumia (Smartphone, Tablet & Laptop), Smartphone nilikuwa naiunganisha na bundle la Internet, vilevile kwenye Tablet na pia kwenye Laptop nayo nilikuwa natumia modem nayo nilikuwa naiunga kwenye bundle. kwa sasa vifaa vyote naviunga kwenye hiyo Router na uzuri wa hii router inakaa na chaji kwa masaa 6 na speed ya internet ni nzuri sana sehemu yoyote yenye mtandao. Kitu kingine kilichonifanya ninunue WiFi Router kuna eneo nilikuwa ambapo palikuwa hakuna 3G, nilitumia zaidi ya dakika 15 kuattach document tena lenye MB ndogo kwenye e-mail ili nitume lakini sikufanikiwa kwa kutumia Modem, bahati nzuri mwenyeji wangu nilimwambia akaniambia tumia WiFi, nikaunga kwenye WiFi yake yaani hata dakika haikufika lile file likawa attached