mkuu nimeandika wana JF then nikasema hasa mlila lakini sikumaanisha kwamba wengine sintapokea mawazo yao anyway naomba niifute kauli yangu na nawaomba radhi wana JF kwa usumbufu uliojitokeza.kama unaomba ushauri usitaje mtu direct kama unamtaka MALILA unge-MP sasa hapa wengine kukushauri wataona wanajipendekeza wakati unamtaka zaidi malila na ndio utakayemuamini.
Wakuu wa JF hasa MR. MLILA
Nataka kuanzisha kilimo kikubwa cha alizeti, kutokana na soko lake kuwa la juu sana hapa nchini nimeona ni muda muafaka nijikite huko na sitakuwa hapa mjini kwa muda kuanzia November mwaka huu.
Nina maswali machache tu ambayo inabidi niyatafutie majibu yake kabla ya kuaza zoezi hili.
1. Ni mkoa upi unafaa kwa kilimo cha Alzeti
2. Je kuna mbegu aina ngapi za Alzeti na ipi itanifaa katika mkoa tanjwa?
3. Nina uhakika na masoko ya ndani, je kuna mtu anafahamu masoko ya nje maana nitalima si chini ya hekari 100 kwa kuanzia.
4. Wazo langu linaendana na kupata mashine ya kukamulia Alzeti hiyo na Packing - je kuna mtu ana fununu za mashine hizi na bei zake hasa za India na china?
Kilimo ni kwa vitendo si maneno: Natoa hoja.
Dr wa Ukweli kachanganya majina kati ya Malila na Mlila, aliyeombwa kuchangia mada zaidi ni Mlila.
Mimi Malila kama mjumbe nichangie kama ifuatavyo. Alizeti inalimwa sehemu kubwa ya nchi yetu, napenda kukupa majina ya maeneo yafuatayo yanayolima sana alizeti na sababu zake.
Idodi Iringa/Mtinko singida/Mby Vijijini/Morogoro/Kibakwe Dom/Chunya,Wanda Singida, huko alizeti inalimwa sana na biashara imeanza huko siku nyingi, usafiri upo, manpower ipo na wanunuzi wa jumla wapo.Haya ni maeneo ambayo unaweza kupata ardhi kubwa sehemu moja kwa bei nzuri sana. Maeneo ya kanda ya kaskazini kama Babati/Hydom/Kilu six huko au Arusha na Moshi, kupata ardhi kubwa huko ni suala gumu kidogo,maeneo kama Handeni/Kilindi kuna ardhi kubwa,bei pia imesimama juu kidogo,vitapeli uchwara vipo. Kiteto ardhi ipo mbugani,lakini mvua zake ni za mashaka sana.
Songea kuko vizuri, lakini kupata eka 100 ni mziki kidogo. Maeneo niliyopendekeza yana mashine nyingi za kukamulia alizeti zinazofanya kazi sasa na hivyo kuongeza ushindani.
Majibu ya Kanyagio hapo juu ni sahihi kabisa.
Project inaendeleaje?Wakuu wa JF hasa MR. MLILA
Nataka kuanzisha kilimo kikubwa cha alizeti, kutokana na soko lake kuwa la juu sana hapa nchini nimeona ni muda muafaka nijikite huko na sitakuwa hapa mjini kwa muda kuanzia November mwaka huu.
Nina maswali machache tu ambayo inabidi niyatafutie majibu yake kabla ya kuaza zoezi hili.
1. Ni mkoa upi unafaa kwa kilimo cha Alzeti
2. Je kuna mbegu aina ngapi za Alzeti na ipi itanifaa katika mkoa tanjwa?
3. Nina uhakika na masoko ya ndani, je kuna mtu anafahamu masoko ya nje maana nitalima si chini ya hekari 100 kwa kuanzia.
4. Wazo langu linaendana na kupata mashine ya kukamulia Alzeti hiyo na Packing - je kuna mtu ana fununu za mashine hizi na bei zake hasa za India na china?
Kilimo ni kwa vitendo si maneno: Natoa hoja.
Kama nikitaka kulima alizeti kama eka 500 napati wapi eneo kama hilo??
Njoo Iringa vijijini kuna maeneo mwafaka kwa kilimo cha alizeti.
Umesharudi? Ile appointment yetu vipi?