Nataka kujifunza lugha mpya, nianze na ipi Kati ya hizi?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
1:kisukuma - Lugha ya asili angalau nikiwa vijijini napata muda wa kubadili mawazo na wazee kwa lugha asilia ( pia asiyekubali kwao ni mtumwa)
2:kihispania - ni mpenzi wa Barcelona, nafurahi sana wale jamaa jinsi wanavyoongea, hii inaingia kama lugha ya burudani. Natamani kuangalia mechi kwa lugha hii maana wale watangazaji huwa wananikosha japo huwa sijui wanaongea nini. Pia ni lugha kubwa duniani
3: Kiarabu, ni lugha Nzuri, pia ni watu waliokaribu sana na sisi kimahusiano, huwa napenda kujua maana pia wenda Kuna maarifa nakosa kwa kikwazo cha lugha, pia naona Raha kwa sababu Kuna wabongo wengi wa kuongea nao. Pia inaonekana ni lugha nyepesi.

4: kigiriki - huku kutanisaidia kutanua ubongo na pia ni lugha mama ya lugha nyingi ulaya, pia ndio original lugha ya bibilia ninayoamini hasa agano jipya itasaidia kutanua uelewa wa mambo mtakatifu,

Nimeweka malengo mwaka huu nijifunze lugha mpya. Kuna faida kujifunza lugha mpya maana is the best mental and brain exercise.
Msaada
Toa ushauri ipi itafaa kwa uzoefu wa kujifunza lugha
Changamoto zake ni zipi
Weka source au hata mbinu itakayonisaidia kufanikiwa kirahisi
Ugumu usiwe sababu ya kutopendekeza maana ninapenda vitu vigumu na vyenye changamoto ili kukuza fikra na bongo
Au ushauri wowote.

Nitajifunza kama hobby ninapokuwa na nafasi...
 
Jifunze Kunena kwa lugha maana utaongea na Malaika na ina lugha zote ulizotaja.
Ni language Bundle hyo
 
¿Quieres hablar Español?, tumia App iitwayo DUOLINGO ni nzuri kwa wanaoanza kujifunza (beginners) na inakuwezesha kukufundisha misamiati mipya ikiendana na sarufi (grammar) pia. Unaweza kuipakua kwa kuitafuta kwenye Google Play (Android) au App Store (IOS) kwa kuandika Duolingo kwenye 'search' na kuipakua bure. Pia unaweza kuingia hapa www.duolingo.com Mimi ninajifunza pia kwa kupitia App hiyo.

Ili kujifunza lugha ya Kisukuma, jichanganye na watu waongeao lugha hiyo na ujibidishe katika kujifunza. Ni rahisi sana sana ukiwa na waongeaji karibu, vinginevyo ni ngumu kwa sababu haina vyanzo vya kutosha mtandaoni kwa ajili ya kujifunza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom