Nataka kufanya biashara ya dagaa wa Zanzibar

Nataka kufanya biashara ya dagaa wa Zanzibar

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,177
Reaction score
734
Habari zenu wana harakati!

Nimevutiwa na biashara ya dagaa wakavu kutoka Zanzibar, sasa ndo naandaa plan ya biashara hiyo. Nataka ifanyia hapa Dar, maeneo ya masoko ya Kariakoo, Ilala, Temeke, Mbagala n.k.

Naomba kwa mtu mwenye mawazo ya biashara hii anisaidie ili nipate business plan ya uhakika juu ya mtaji, soko, maeneo ya kupata bidhaa zanzibar, gharama zake na ikiwezekana hata wadau walio katika biashara hii nishirikiane nao.

Natanguliza shukrani!
 
Mimi niliko ndio kiwandani ukihitaji kwa jumla nione mimi niko Kizimkazi Zanzibar.
 
Msaada: dagaa wa Znz ndo wanakuaje?,Wana tofauti gani na wanaovuliwa DSM, Mtwara, Tanga n.k ikiwa bahari ni moja?
 
Msaada: dagaa wa Znz ndo wanakuaje? wana tofauti gani na wanaovuliwa DSM, Mtwara, Tanga n.k ikiwa bahari ni moja?

Hawa jamii moja na wa Dar, sabab wote huvuliwa bahari ya hind hujulikana kama Dagaa mchele ila kule Zanzibar wanawaandaa kwa ubora zaidi kwa kuwapika na kuwaongezea vikolombwezo

Hivyo huwa watam, tofauti na Dagaa wa Dar
 
Back
Top Bottom