Nataka kuanzisha jarida

dully santo

JF-Expert Member
Apr 12, 2014
260
334
Habari zenu wapendwa, hope mko poa.

Nimekuja mbele yenu nahitaji kusaidiwa kimawazo na kupata connection.

Kuanzia mwaka jana mwezi wa 8 nilianza kufanya research kuhusiana na Tatizo la dawa za kulevya, nilichogundua kuwa kwanini utumiaji huo wa dawa haupungui/kuisha kabisa ni kwamba elimu kuhusiana na athari za dawa za kulevya ni mdogo, watu wengi hawajafikiwa na elimu hii.

Hivyo nikaamua kuja na wazo la kuanzisha magazine ambayo itakuwa na mfumo wa katuni ambazo zitakuwa na ujumbe kuhusiana na athari za dawa za kulevya.

Hii ni kampeni lkn kampeni hii itafanyika kwa njia ya mchoro kupitia magazine ambazo zitakuwa zinatolewa bure (Jina la kampeni hii nishaandaa).

Tayari nimeshaandaa team akiwemo mchora katuni na msanifu picha. In short process zote za awali nishakamilisha, changamoto iliyopo mbele yangu ni kupata kampuni ya kufanya nayo kazi.

Nimekusudia kufanya kazi hii na makampuni ya magazeti (kati ya Mwananchi au Nipashe) ambapo mtu akinunua gazeti anapatiwa magazine yake inayohusu athari za dawa za kulevya.

Nakusudia pia baadae kuanzisha radio show ambayo itakuwa rahisi kusikilizwa na watu wengi tofauti na tv.

Hivyo ndugu zangu naombeni msaada wa kimawazo au kama kuna accessibility ya kukutanishwa na viongozi wa makampuni tajwa hapo juu itakuwa vizuri.

Ahsanteni.
 
ni wazo jema sana waendee hao magazeti watakupa mwongozo huo halafu ni vyema sasa ukafungua jarida lako pembeni la kushauri na kuweka hamasa kwa suaala hilo la madawa ya kulevya
 
Wazo hilo hauwez kupata support toka makampun bnafs koz halina faida yoyote!
Labda wazo lako uliweke vzur komaa na serkali na NGOs za ndani au kimataifa wakupe support
Ila lazma uonyeshe juhud zako kwanza kwa gharama zako
Jipange
 
Usipoamka utakufa masikini, hilo ni wazo adimu la mabilioni mkuu Wake up
 
Back
Top Bottom