Nataka kuajiri body guard, je sheria za utumishi wa umma zinaruhusu?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,895
19,069
Mimi ni mtumishi wa umma ila junior level. Nataka kuajiri armed bodyguard wa kunilinda ila sijajua sheria za utumishi wa umma zinasemaje kuhusu hilo.

Nimejaribu kuzipitia sijaona katazo la mtumishi kuwa na ulinzi wake binafsi, najua siko entitled na ulinzi wa serikali ila nataka kuajiri mlinzi wangu.

Hiki kipindi cha sikukuu nilicontract kampuni moja ya ulinzi kunilinda, wakanipa kijana ambae ana leseni ya kutembea na bunduki, pisto.

Mkataba wangu na wao umeisha ila nataka kuajiri mlinzi wangu binafsi wa kunilinda muda wote nikiwa kazini, kwenye daladala na hata nyumbani mwenye bunduki.

Najua kuna watu wanajua hayo mambo humu, je ni sahihi au sio sahihi?
 
Ungekuwa unatafuta bodgurd wa kumlinda mkeo ningekupa ufafanuzi....sasa wa kukulinda mwenyewe subiri wajuzi waje...
 
Mkuu,mbona una hofu kiasi hicho? Mlinzi mpaka kwenye daladala? Wewe ni Tapeli unaogopa kufanyiziwa?
 
Jamaa inasound kama msukuma aliepata ela baada ya kuuza mashamba na ng'ombe wote wa urithi.. #justsaying ngoja watakuja wadau apa kama sio ushauri utapata huyo bodyguard kabisah humu humu JF
 
Niliwahi kuuliza hapa, wale walizi binafei wa wanasiasa haswa wagombea uraisi, mfano yule aliyekuwa akimlinda mama wa ACT, aliyekuwa akimlinda wa Chadema, na wa Ccm, n.k. wale huwa wanakuwa ni usalama wa taifa ama ni binafsi tu wenye leseni? Akijibiwa jamaa hapo, nami mnisaidie kunijuza. Niwie radhi mtoa post kama nimeingilia post yako.

Ahsante!
 
Kuna Mwanasiasa mmoja nchini Kenya, ni Meya wa Nairobi naamini, Mr Sonko. Yeye ni anaitumikia Serikali na ana walinzi wake binafsi, tena wapo full armed. Sasa sijui sheria za utumishi za wenzetu jirani Kenya ni tofauti na sisi?! Kuna ulazima wanaofahamu haya watujulishe.

Ahsante!
 
Niliwahi kuuliza hapa, wale walizi binafei wa wanasiasa haswa wagombea uraisi, mfano yule aliyekuwa akimlinda mama wa ACT, aliyekuwa akimlinda wa Chadema, na wa Ccm, n.k. wale huwa wanakuwa ni usalama wa taifa ama ni binafsi tu wenye leseni? Akijibiwa jamaa hapo, nami mnisaidie kunijuza. Niwie radhi mtoa post kama nimeingilia post yako.

Ahsante!

Au kama yule mlinzi wa Diamond Platnumz!
 
Unataka mlinzi ambaye muda wote utakuwa naye hivi.
images
 
Unataka mlinzi ambaye muda wote utakuwa naye hivi.
images
Huyu wa daimond sio mlinzi bhana, huyu atakuwa msaidizi wake kwajinsi anavyo onekana kwenye picha,mlinzi gani anabebeshwa adi mabegi kiasi hicho? Kama kuna mtu anataka kumdhuru bosi wake adi atupe apo mabegi bosi siatakuwa kashavimba vyakutosha?
 
Back
Top Bottom