Nipo pamoja nawe kama usemi wako ni dhahiri,ila wasiwasi wangu ni kuwa ukishalambishwa halua utanywea,ila kama wewe ni ngangari alutacontinua.Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Greeque atleast hapo tayari tunajua tatizo, na malengo ni kubadilisha na nina uhakika tutafanikiwa, huku pengine hata hayo uliyosema hayaonekani.
Burn,
tatizo si kuwa na kadi ya CMM na kujiunga na Kina Slaa,Je utakisaidia vipi CHAMa?
karibu CCM
Jamani huyu anataka kadi ya CCM rasmi, maana ameona CCM ya sasa hivi si rasmi. Niliwahi kusikia kuwa kuna CCM mtandao, CCM Asili, etc na sasa Burn amekuja na CCM Rasmi.Nataka kadi ya ccm rasmi
Kwa hiyo Mazee Burn unategemea utaenda kukisafisha Chama kutoka kwa Mapapa na Manyangumi ya Ufisadi, angalia tu wasije wakakubadilisha.
Greeque atleast hapo tayari tunajua tatizo, na malengo ni kubadilisha na nina uhakika tutafanikiwa, huku pengine hata hayo uliyosema hayaonekani.