Natafuta wanunuzi wa kuni kwa jumla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta wanunuzi wa kuni kwa jumla

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ROKY, Sep 27, 2011.

 1. ROKY

  ROKY Senior Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hi wana JF wote,
  Natafuta watu wa kununua kuni za jumla.
  Nina shamba jipya nalisafisha, hivyo kuna miti mingi sana kwa ajili ya kuni.
  Eneo lilipo shamba hilo ni mkoa wa Pwani, umbali wa kilometa 100 toka DSM.
  Bei ya kuni ni maelewano tu na wanunuzi.
  Wana JF naomba mnipe contacts za wanunuzi watakaonunua kuni hizo kwa jumla.

  Thanks in advance.
   
 2. babalao

  babalao Forum Spammer

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tangaza kwenye gazeti la Nipashe matangazo madogo madogo utapata soko
   
 3. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaribu pia kuwasiliana na uongozi wa canteens za vyuo mf. Ardhi au UD. Hawa pia ni watumiaji wazuri wa kuni, suredly you'll get a delicious market.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Huwezi zichoma kuwa mkaa utakuwa umetengeneza faida zaidi
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hivi huu uharibufu wa mazingira bila aibu????/
   
 6. ROKY

  ROKY Senior Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Huu sio uharibifu wa mazingira. Kinachofanyika hapa ni matumizi ya miti inayoondolewa kwenye shamba ili kupisha kilimo.
  Kama nilivyosema kwenye post yangu, "ninasafisha shamba jipya", na katika usafishaji wa shamba jipya, ambalo kwa sasa ni pori, lazima kuna miti itakatwa ili kupata eneo la kilimo. Sasa miti kama hiyo ndio naitafutia soko ili itumike kama kuni badala ya kuichoma moto na kuipoteza bure.
  Hapa hakuna uharibifu wa mazingira.

  Wana JF naomba mwenye contacts za wanunuzi wa miti kwa ajili ya kuni anipe.
   
 7. v

  valid statement JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  jaribu kwenye sekondar skul.wananunuaga .
   
Loading...