Kuna mama ana duka la spare za mazda na ford pale tabata. Kama unatoka ubungo, ukishapita mataa yanayokwenda tabata, endelea kama unaenda buguruni angaliaa upande wa pili wa barabara yaani unaotoka buguruni kuja ubungo, utaona kuna kituo cha basi na nyuma/pembezoni mwa hicho kituo kuna duka kubwa la pale blue limeandikwa mazda na ford... Unaweza kupata au kumuagiza akakuletea ndani ya muda mzuri...ila ana bei sana... Anasema vitu vyake vyote ni genuine... (Sina uhakika na siwezi kuthibitisha) japo binafsi nimeshanunua air cleaner ya Mazda MPV...
By the way, hiyo tribute ni auto au manual? Vipi unaweza kunipa mrejesho wake kidogo, kwani nafikiria kuichukua 2.0 manual...ila nikifikiria spare ndio nasita.