Natafuta soko la kuku wa kienyeji

Natafuta soko la kuku wa kienyeji

CHRISTURKER

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2012
Posts
267
Reaction score
55
Nimefuga kuku wengi wa kienyeji, ningependa kupata soko la uhakika hasa miji ya Dar, Moro na Dom.Naweza kukuletea mahali ulipo kwa order ya kuku wengi. Kuku wangu ni wenye afya na wamechanjwa kuwakinga na magonjwa mbalimbali.Kwa mawasiliano piga 0765 829257 au tupia PM hapa
 
Wengi wangapi? Unaweza sema wengi kumbe unao 500 tu. Malizia kabisa uko mkoa/location gani mkuu. Ungeweka na bei ya jumla kabisa, ikiwezekana na uzito wa kuku wako.
 
Wengi wangapi? Unaweza sema wengi kumbe unao 500 tu. Malizia kabisa uko mkoa/location gani mkuu. Ungeweka na bei ya jumla kabisa, ikiwezekana na uzito wa kuku wako.

Mkuu daah, umenishangaza hapo kwa red, kumbe mimi mwenye 40 hata chichemi!!!!
 
Mkuu daah, umenishangaza hapo kwa red, kumbe mimi mwenye 40 hata chichemi!!!!

Kuku 40 ni supu ya siku moja pale River side Ubungo, sasa ukiomba tender ya kupeleka kuku pale itakuwaje?

Inabidi mtu utangaze kuanzia kuku 1000 ili upate mteja mkubwa, najaribu kuonyesha vile wakulima wa Bongo tunavyokosa masoko ya maana kwa sababu tunakuwa na supply isiyo stable. Hapo ndio inakuja haja ya kuunganisha nguvu ili tuzalishe kwa wingi na kuweza ku-supply kwa uhakika.
 
Fanya hivi.au jibu haya maswali

1.Ninao kuku .................
2.Nipo mkoa wa..............wilaya ya..............kata ya.................
3.kila kuku ni sh....................,ukichukua kuanzia 20 kila @ ni sh...............
4.wasiliana nami kwa simu no........................ nk
 
Mimi niko njiani kufuga kuku wa kienyeji/chotara, na kuwatunza kama inavyo takiwa ili wawe na afya nzuri, au tuseme nimesha anza kidogo ya majaribio lakini linalo nisitisha ni soko, je soko kweli lipo. Lengo langu ni kufuga kuanzai kuku 1000 kwa mwezi ili supply iwe kwenye kuku 1000 kwa mwezi ikiwezekana zaidi, nina fuga nje ya mkoa wa DAR (tanga).
 
Tanga bei zikoje? Hakuna soko?
 
Mkuu daah, umenishangaza hapo kwa red, kumbe mimi mwenye 40 hata chichemi!!!!

kuna mchoma chipsi hapa mtaa wa pili anachinja kuku 60 kwa siku!! kuna watu wana tender kupikia harusi, seminar, nk. hao wako hata freezer ndogo hawajai.
 
Back
Top Bottom