Mmh kwa hiyo bei, sioni namna unaweza ukapata kirahisi Boxer ambayo haijachoka. Boxer mpya(Brand new, zero km) sio chini 2ml, Used(Imetumika sio zaidi ya mwaka mmoja, Ingine haijapigwa spana au haijawahi kupigishwa bodaboda) sio chini ya 1.5ml.
BOXER ILIYOCHOKA: Boxer yoyote uliyopigwa boda boda zaidi ya mwaka mmoja, au Iliyotumika rough road kwa zaidi ya mwaka mmoja, au Iliyowahi kupiga mzinga(Kupata ajali mbaya) au Engine imepigwa spanner, hiyo unaweza kupata hata kwa 1ml, lakini ni majanga, yaani ni bora ukanunua mpya kabisa.