Habari zenu wadau?
Naomba msaada.
Natafuta paka (domestic cats) wawili - dume na jike.
Wasio na mabaka kama ya chui.
Wenye mabaka kama ya chui wana asili ya kuwa deviant (paka mwitu)- huwa na tabia ya kukamata vifaranga na hata kuku.
Nawahitaji sana, panya wananisumbua.
Sipendi kutumia sumu au mitego - ni kinyume na taratibu za mazingira, pia hazimalizi tatizo - hupunguza tatizo tu.
Njia sahihi ni kufanya mazingira yasiwe rafiki kwa panya (i.e kutoacha mabaki ya vyakula hovyo au kutohifadhi vibaya vyakula) na biological control (kwa kutumia paka).
Natanguliza shukrani