Natafuta nafasi ya kufundisha Mathematics

jivinga

Member
Jun 23, 2016
17
5
Ndugu wana jf. Natafuta nafasi ya kazi ya kufundisha. Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu katika degree ya ualimu katika masomo ya hesabu na jiographia. Nimekuwa nikifundisha secondary advance na nimefaulisha vizuri sana wanafunzi kwa idadi kubwa kwa mda mrefu. Ila maslahi pamoja na mazingira ya kazi yalikuwa si mazuri sana. Hivyo nimeamua kutafuta sehemu nyingine ambayo inaweza kuwa na maslahi mazuri zaidi. Ninauwezo wa kufundisha sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na pia ninauwezo wakufundisha collage . Kwa maelezo zaid pamoja na cv zangu naomba tuwasiliane inbox au namba hii 0744704597.
 
Ndugu wana jf. Natafuta nafasi ya kazi ya kufundisha. Mimi ni mhitimu wachuo kikuu katika degree ya ualimu katika masomo ya hesabu na geographia. Nimekuwa nikifundisha secondary advance na nimefaulisha vizuri sana wanafunzi kwa idadi kubwa kwa mda mrefu. Ila masirahi pamoja na mazingira ya kazi yalikuwa si mazuri sana. Hivyo nimeamua kutafuta sehemu nyingine ambayo inaweza kuwa na masirahi mazuri zaidi. Ninauwezo wa kufundisha sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na pia ninauwezo wakufundisha collage . Kwa maelezo zaid pamoja na cv zangu naomba tuwasiliane inbox au namba hii 0744704597.

Mkuu, sijui kama unafanya kusudi au la. Hayo maneno niliyoyapiga nyekundu ni kweli hujui usahihi wake? Sisemi kuwa hujui ila kwa makosa ya kiuandishi kama hayo yatakupa wakati mgumu sana hasa kwa human resource managers wanaopita humu.
Mwalimu ni kioo cha jamii, sasa kama wewe ni mwalimu tena wa hesabu unateleza namna hii, je, hao utakaowafundisha tutegemee nini?

Sina nia mbaya isipokua nakukosoa kukujenga ili kukuwekea mazingira ya kutofanya makosa hata utakapoitwa kwenye interview.

Niwie radhi kama hujapendezwa na ukosoaji wangu ila huo ndio ukweli kwamba aina ya maneno unayoyatumia huyatumii kwa usahihi.
Kila laheri ktk kufanikisha maombi yako.

Badala ya maneno hayo mekundu hebu tumia haya hapa upate 'uroda' wa lugha:
1. geography au jiografia
2. masilahi
3. college
 
masirahi ni ndo nini? kwa namna hii unaweza kuwalisha matango pori watoto wetu
Mimi mpaka naogopa hiyo elimu na maarifa watakayopewa watoto wetu na aina ya walimu kama huyu. Yani toka darasa la kwanza mpaka la tatu hakujua kusoma na kuandika kwa ufasaha???
R.I.P. Elimu ya Tanzania.
 
Mkuu, sijui kama unafanya kusudi au la. Hayo maneno niliyoyapiga nyekundu ni kweli hujui usahihi wake? Sisemi kuwa hujui ila kwa makosa ya kiuandishi kama hayo yatakupa wakati mgumu sana hasa kwa human resource managers wanaopita humu.
Mwalimu ni kioo cha jamii, sasa kama wewe ni mwalimu tena wa hesabu unateleza namna hii, je, hao utakaowafundisha tutegemee nini?

Sina nia mbaya isipokua nakukosoa kukujenga ili kukuwekea mazingira ya kutofanya makosa hata utakapoitwa kwenye interview.

Niwie radhi kama hujapendezwa na ukosoaji wangu ila huo ndio ukweli kwamba aina ya maneno unayoyatumia huyatumii kwa usahihi.
Kila laheri ktk kufanikisha maombi yako.

Badala ya maneno hayo mekundu hebu tumia haya hapa upate 'uroda' wa lugha:
1. geography au jiografia
2. masilahi
3. college

Kwa kweli mimi kama mzazi nitapata kigugumizi kumkabidhi mtoto wangu kwa mwalimu kama huyu. I am sure a smart form 2 student will have no difficulty spelling those words correctly!
 
Kwa kweli mimi kama mzazi nitapata kigugumizi kumkabidhi mtoto wangu kwa mwalimu kama huyu. I am sure a smart form 2 student will have no difficulty spelling those words correctly!
Yeye ataona kama tunamvunja moyo lakini ukweli ni kwamba anatia mashaka uwezo wake kama mwalimu. Mimi namshauri atafute mtu anayezimudu vizuri lugha za Kiswahili na English ampige msasa angalau kwa miezi miwili ndipo aanze tena kufanya maombi ya kazi.
 
Kinachoniumiza zaidi ni kwamba walimu wa aina hii wapo wengi sana tena huyu ana nafuu.Jaribu kupitia nyuzi zinazokutanisha walimu,tunaelekea kubaya sana.
 
Kinachoniumiza zaidi ni kwamba walimu wa aina hii wapo wengi sana tena huyu ana nafuu.Jaribu kupitia nyuzi zinazokutanisha walimu,tunaelekea kubaya sana.
Mkuu nakubaliana na hoja yako 100 kwa 100. Siku hizi walimu wa siku hizi walio wengi wamekua wa kutilia mashaka. Jiulize walimu wanaokosea uandishi wa baadhi ya maneno watakavyoharibu kabisa ubora wa elimu kwa watoto wetu miaka kadhaa ijayo.

Mfano:
neno thibitisha linapokosewa na kuandikwa dhibitisha inakera, inahuzunisha na kuleta hofu kubwa ktk ubora wa elimu yetu nchini.
Sijui tutatokaje hapa?
 
Ndio Fungua Tuition Sasa utapata "masirahi" mazuri na utamenage wakati wako namna unavyopenda mwenyewe.
 
Kinachoniumiza zaidi ni kwamba walimu wa aina hii wapo wengi sana tena huyu ana nafuu.Jaribu kupitia nyuzi zinazokutanisha walimu,tunaelekea kubaya sana.
Hahahaha.
Mkuu wewe usiseme nyuzi za humu tu, na pia siyo walimu tu. Nenda makazini wanaojiita graduates, wengi wao ukimwambia akuandikie technical report kila mwisho wa mwezi, utajuta. Hata kama muda wako hautoshi inabidi ufanye na kazi zake. Wanatia aibu. Grammar ni shida. Iwe ya Kiswahili au Kiingereza bado ni lugha gongana. Hapo ukiangalia trascript yake ana GPA 4.0 just imagine, aliipataje? ni swali la kujiuliza mara mbili mbili. Watalalamika kuwa hakuna ajira, lakini kwa uandishi huu. Hata kuwa shortlisted tu inakuwa taabu. Sasa fikiria huyu anasema anaweza kufundisha chuo, sijui chuo cha aiana gani hicho kinaweza kumchukuwa mtu kama yeye kama uandishi wake tu unatia shaka.
 
*TANGAZO TANGAZO*

Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka mkoa wa Kagera *(KAUSTA)* unapenda kuwatangazia nafasi za kujitolea kufundisha katika shule za *kata* mkoani Kagera wanavyuo wote wanaotegemea kuhitimu kuanzia mwezi huu wa saba.KAUSTA itatoa posho ya *Tsh. 200,000* kwa mwezi. Umoja huu utawahudumia walimu wote watakaopata nafasi hiyo kwa huduma za *chakula, malazi kwa kipindi chote wawapo vituo vya kazi vya kujitolea*.

Walimu wanaohitajika zaidi ni wa masomo ya *Chemistry, Mathematics, Physics, Biology, English na Geography
Muda wa kujitolea ni miezi *6-8*kuanzia mwezi wa nane mwaka huu.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18/7/2016.

Kwa maelezo zaidi piga namba zifuatazo 0766174514 na 0783644221.

Imetolewa na

Amos Muzee
Mratibu wa KAUSTA
Mkoa wa Kagera.
 
Nashukuru kwa malekebisho yenu. Lakini ujumbe si mmeulewa?? Au mnataka tu kukuza mambo??
Wengine mko kufuatilia gramatical errors za watu tu kama umeuelewa ujumbe naikiwa hunamsaada ni bora kufanya mambo mengine. Ukawaachia wenye mawazo ya kujenga
 
Wengine mko kufuatilia gramatical errors za watu tu kama umeuelewa ujumbe na ikiwa hunamsaada ni bora kufanya mambo mengine. Ukawaachia wenye mawazo ya kujenga
 
jivinga, nakueleza kiungwana kabisa kama hayo ndiyo majibu yako itakupa shida sana kupata hizo kazi na hata ukizipata bado utajikuta unachukia kazi. Naomba kuwasilisha.
 
LAKIN INATAKIWA IELEWEKE KWAMBA HUYU SI MWL WA LUGHA YA KISWAHILI WALA ENGLISH
Sawa tunakubaliana si mwalimu wa masomo hayo, je, hizo notes za somo atakalofundisha ataziandika kwa usahihi au ndo mwanzo wa kuwamezesha watoto wetu "broken" za kutosha?
 
Ok!! thanks odili for your advice . Let me continue with searching of a vacancy one day yes!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom