Hakuna mwanamke ama mwanaume tasa. Sayansi imeshindwa kuestablish sababu ya mimba kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kwa sababu hiyo kuna watu wameishi 10 yrs na wenza wao na wakaitwa tasa, wakakutana na wenza wengine na kupata watoto.
Kwa umri uliotaja sijui utahakikishaje huyo mwanamke ni tasa. Ukizingatia kuna watu wamepata ujauzito at 50 yrs of age.
ndugu una haki ya kutafuta mwanamke umtakaye! Lakini nahisi hujatenda haki kwa kutoweka maelezo yako binafsi kama kweli uko serious. Angalau mwambie huyo tasa unayemtaka kwamba wewe nawe pia ni tasa (pengine) au unao watoto umezaa na wanawake tofauti-tofauti, au unao watoto wa mama mmoja ila umeachana naye kwa sababu fulani-fulani, au ulikuwa umeoa mwenzio akatangulia mbele za haki, umri wako, n.k.
Hapo utaonesha unajua unachotafuta na hakika utampata humu humu wamo tu. Inawezekana hutaki tasa bali unataka asiyetaka kuzaa tena (yaani anao watoto/mtoto) na hana mume na anataka mume mwenye watoto wake tayari hataki mwanamke anayetaka mtoto.., fungukaaaa