Natafuta mume anayeishi Dar

Hadi namba umeweka duu kweli upo seriously sio wale wengine wanahitaji mume alaf ukiwafwata pm wanakutolea matusi makubwa makubwa ya nguoni ... kwa vile vijana tuliokoka tupo basi ngoja tujaribu izo namba
 
Mmh hivyo vigezo!! Angalia baada ya miaka mitatu usirudi hapa na kusema natafuta mume yeyote, ilimradi mwanaume anayevaa suruali.
 
namba imeandikwa bado watu wanasema nifuate inbox...
NB:anatafuta mwanaume wa dar!!
 
mungu akupe hitaji la moyo wako!nna vigezo vyote but nipo mkoani!!!
 
mlokole utafute mchumba kwa macho ya nyama!Wenzio wanaenda kiroho zaidi napata hofu
 
Hakuna mwanaume ambae hana tatizo la kibiologia wala kifizikia mwenye umri wa miaka 34-38 hakawa hana mtoto na hajaoa nadhani ungetoa kigezo cha kuto kuwa na mtoto kwa umri huo

Wapishe wenzio tafadhali usitusumbue!
 
Waaume wa Dar es salaam ndo maana tunaambiwa tuna matatizo!!! mtoto amesha kuwekea namba ya simu hapa kwenye bango, harafu unaleta mbwembwe eti akufuate inbox!!!
unataka umwombe vocha??

samahani kuna usemi mume mwema huletwa na bwana, vipi katika maombi yako hujaletewa bado? toa hayo masharti maana kwa kuangalia mashart yako inawezekana ndiyo maana hujaletewa. muombe Bwana mume na umsimwekee mashart ya aina ya mume unayemtaka.
 
SIFA HIZO NINAZO ILA MOJA TU ULIVYOSEMA WEWE NI MLOKOLE BASI TENA SINA IMANI NA MLOKOLE YEYOTE DUNIANI NILISHAUMIZWA INATOSHA HONGERA KWA KUTOA NAMBA YAKO YA SIMU UNAONYESHA MSISITIZO MUNGU AKUBARIKI ILA HATA HIVYO UMEONYESH UBAGUZI KWA WATOTO USIO WAZAA WEWE IKO WAPI IMANI YAKO YA KILOKOLE??? MTU MPAKA ANAFIKISHA UMRI WA MIAKA 38 HANA MTOTO LAZIMA NAYE ATAKUWA NA MATATIZO KAMA WEWE.
 
Hongera mama jitahidi wapo.
 
Utofauti wa maisha unakuja hapa binti aliye soma mpaka la saba/kidato cha nne anachumbiwa na ndoa anafunga kwa nderemo na vifijo.Binti Aliye soma mpk kidato cha sita/chuo kikuu anatafuta wa kumuoa anamkosa,Hii ina maana gani? Ina maanisha wanaume hatuowi makaratasi mnayo yapata darasani tunaoa mwanamke mwenye staha na future mengine ni additional advantage.Dada endelea kumuomba Mungu atakujibu muda ukifika acha humu JF wengi wapitiaji tu.
 
Hakuna mwanaume ambae hana tatizo la kibiologia wala kifizikia mwenye umri wa miaka 34-38 hakawa hana mtoto na hajaoa nadhani ungetoa kigezo cha kuto kuwa na mtoto kwa umri huo
Unaishi dunia gani? Mbona wapo wengi tu hawataki watoto wala kuoa.
 
Siku hizi ni rahisi kujua namba ya simu ni ya nani, especially tigo line. Nimeangalia nimeona hii namba ni ya mwanaume jina linaanzia R sasa dada yetu hadi hapo vibendera vyekundu vinaanza kupaa!
 

Pole naona majibu mengi ya kukukatisha tamaa ila usijali na usikate tamaa. Endelea kuomba ili hao wanaokuja upate kupata yule uliyekusudiwa . Songa mbele bila kujali majibu unayopewa ya kukatisha tamaa , utapata tuu maana wako walio makini na uhitaji humu ndani kama wako . Kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…