Natafuta mshirika wa kibiashara

Eng Jay

Member
Sep 11, 2019
17
14
Mimi ni Engineer mwenye Elimu ya Kiwango cha Masters, Nakaa DSM Natarajia kuanzisha biashara ambayo partly inahusu fani yangu. Nimefashafanya kazi ya awali ikiwa ni pamoja na utafiti, mpango wa biashara na ujenzi wa miundombinu. Kimsingi kazi za awali zimekamilika kwa kiwango cha 60%

Nahitaji mshirika wa biashara ambaye atatoa kiasi cha tsh 60m au zaidi kutegemea na kasi ya expansion ya biashara yetu. Lakini mil 60 ndo kiwango ambacho kitatuwezesha kuingia sokoni na kuanza operations. Kwa mujibu wa business plan, fedha hizo zinahitajika kwa miezi minne kwa kiwango cha 15m kwa mwezi. Biashara inategemea kuanza kujiendesha baada ya miezi 4, na faida kuanza kupatikana baada ya mwaka mmoja kulingana na nguvu tutakayoweka.

Kwa maelezo zaidi tuma PM, ili tupeane mawasiliano ya simu na email kwa ajili ya kuelezana biashara kwa kina. Mshirika hatalazimika kufanya kazi, lakini atapewa uhuru wote wa ku monitor biashara inavyokwenda. Maswala yote ya kisheria yatazingatiwa.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom