Natafuta mchumba wa kike mkazi wa Dar es Salaam

NatGeo18

Member
Jan 12, 2020
10
7
Heshima kwenu wakubwa kwa wadogo,

Nimefikia uamuzi wa kujiunga baada ya kuelezwa na jamaa yangu wa karibu ambaye ameweza kupata mwenza kupitia mtandao huu. Lengo langu ni kutafuta mwenza, nikipata hitaji langu sina nia ya kuendelea kuitumia a/c tena.

Kama bandiko linavyojieleza, ninatafauta mchumba wa kike anayeishi Dar es Salaam.
Sifa ninazohitaji kwake:
a) awe muislam
b) awe miaka 18-25 mwisho
c) elimu si kigezo cha muhimu. kikubwa ajue kusoma na kuandika vema, mwepesi na mwenye dhamira ya kujifunza mambo mbalimbali yenye kuleta tija
d) niwe mkweli napenda sana awe na maumbile makubwa kwa maana awe na makalio. hakna haja ya kuficha hili. sivutiwi na mwanamke asiye na chura.
e) akiwa amesoma dini itapendeza pia. atakua mwenye msaada kwangu maana sijui kabisa mambo ya dini yangu.
f) awe msikivu, mpenda maendeleo, na anayethamini. sitaki mwanamke mambo mengi.

Kuhusu mimi nitamueleza na akivutiwa basi itakua mwanzo wa safari mpya. Ila kwa ufupi, mimi ni mstaarabu sana, napenda kusoma vitabu, napenda sana masuala ya afya na lishe, sinywi pombe wala kuvuta, siendi klabu (na sijawahi)

Nipo serious. PM ipo wazi.

SHUKRANI ZA DHATI
 
.
83307288_1063379007367678_5317371461810257920_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadi hivi leo sijafanikiwa kupata ndugu zanguni.
N'na dhamira ya dhati kabisa.
Bado sijakata tamaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom