ndio kampuni tumesajiri na utaratibu wa share kwa sasa tumegawana baadhi ya share na baadhi niliacha kwa ajili ya wabia/mbia kwahiyo tutapoongea na kufikia makubaliano utapata share zako rasmi.Good idea.
napenda kuwekeza kwenye growing business kama hizi.
mmeshasajili kampuni yenu na kama mmesajili utaritubu wa shares upoje ???
ni kweli kama kampuni hatuna capital ya kutosha ila tunaamini kupitia kazi zetu tutakuza mtaji wetu kwa njia mbalimbali moja wapo ni hii ya kutafuta wabia/washiriki ili mtaji ukue.Mnaanzishaje company hamna capital yakutosha
Tayari hapo inaonyesha wazi mko namadhaifu flani..
-sawa nitafafanua zaidi mkuuKwa kukuongezea tu sio wote humu wanajua Tehama ni nini maana wengine wako nje na wana uwezo wa kuwekeza hata kama hawapo huko
Jaribu kufafanua zaidi ili na diaspora waelewe pia au unahitaji wa nyumbani tu
8m sio nyingi ila je kampuni imesajiliwa na mmejikusanya kiasi gani mpaka sasa na kama hakuna ina maana wote watatu hamna ajira ya mshahara?
Nimekuelewa vizuri, nasubiri wachangiaji na majibu yenu zaidi.-sawa nitafafanua zaidi mkuu
-8 mill. ni kiwango cha chini cha mbia kujiunga na sisi ila anaweza kuja na mtaji mkubwa zaidi na zaidi..
kampuni imesajiliwa na hadi sasa hatuna kiasi cha maana tulichokusanya kutoka na aina ya kazi tunazochukua oda kutoka kwa wateja hatuwezi kuchukua oda au tender kubwa kwa sababu ya mtaji/capital kuwa ndogo..
_kwa wahusuka tuliopo sasa ni mmoja tu ndio mwenye ajira na ni private wengine kampuni ndio maisha yetu tunaitegemea kuendesha maisha ndio maana tunajitahidi kuikuza iwe kubwa.
Bila shaka wewe sio mtanzania, hujui hali ya watanzania au unaleta ujuaji! Jifunze kuwa positive mkuu wangu!Mnaanzishaje company hamna capital yakutosha
?Mpaka sasa mko watu wa 3 Je kuna mtaji kiasi gani mmeweka nyie? Kama mwanahisa mpya anatakiwa kwekeza yy tu 8 million +.
Asante
Kabisaa hizi content ndo zinapaswa ziwepo saana... vijana wafanikiweNa mimi hapa niko kujua feefback.
Sijui kwann nyuz kama hiz huwa hazina wachangiaji ?? Wakat kwa wengine investment ni fursa. Hii inatoa alert kuwa biashara nying za hapa nyumban ziko hati hatini au labda watu hawana ufaham kuhusu hiz mambo
For sure. Mimi nimepitia the period kama huyu mwamba ila nikasema acha nikomae tu mwenyewe. Ni ngumu sana kuwapata hao watu mitandaoni..ngumu mnoooKabisaa hizi content ndo zinapaswa ziwepo saana... vijana wafanikiwe
Nikaona kama fursa kuntu kumbe ni ya kitambo mno.habari zenu wadau
niende moja kwa moja kwenye mada,
mimi ni kijana wa makamo nia ya kuja hapa jukwaani ni kuomba mbia/mshiriki wa kampuni mwenye uwezo wa kuwekeza mtaji wake katika kampuni yetu kwa makubaliano maalumu.
kampuni inajihusisha na mambo ya tehama/ict technology katika sector mbalimbali.
1. kazi na hali ya kampuni kwa sasa.
-kazi tunazojihushisha nazo ni kusuka mifumo mbalimbali ya tehama (ict system), mafunzo ya tehama(ict training) na uuzaji wa vifaa vya tehama kwenye kampuni, mashirika na shule mbalimbali.
-kwa sasa kampuni ipo dar es salaam ila lengo ni kufungua matawi mikoani kwa baadhi ya mikoa baadae mwaka huu
-kwa sasa kampuni kimtaji haipo vizuri
-kimasoko ipo vizuri sana na wateja wapo wa kutosha shida ni mtaji wa kuhudumia wateja ni mdogo sana. (hivyo tunaishia kufanya kazi ndogo ndogo)
-kiujuzi kampuni inawataalm wazuri na wenye weledi sana wa tehama na usimamizi.
2. mahitaji ya kampuni kwa sasa
-mtaji wa kuhudumia oda za wateja mbalimbali (hili ndio hitaji kuu)
-eneo la ofisi na baadhi ya vifaa
-wezeshaji kifedha kwa rasilimali watu (tupo 3 tu kwa sasa )
3. sifa za mbia/mshiriki tunayemuhitaji
- awe na uwezo wa kuweka mtaji kuanzia tsh. 8.million na kuendelea
-aweze kutoa ushirikiano kwenye mawazo katika uboreshaji au kuendeleza na kukuza mtaji
-awe mlezi (mentor)
pia
-tutamruhusu alete mtu wake au yeye mwenyewe asimame fedha
-tutatoa ushirikiano kwa uwazi bila kuficha ficha vitu.
kwa ambaye anaweza kujiunga nasisi kama mbia/mshiriki karibu inbox nawasubiri pia kwa mwenye ushauri wazo karibu kwa komenti zako ni muhimu kwetu.
N.B - nilishawahi kutafuta fedha kwenye taasisi za benki ila usumbufu ni mkubwa na masharti ni mengi sana baadhi sisi hatuna vigezo wanavyotaka. kwenye mikopo ya vijana huko nimejaribu pia ila mlolongo ni mkubwa foleni sio ya leo wala kesho kuisha. nilishawahi kutafuta wabia/kama miezi 3 nyuma ila niliyempata hakuwa serious ni tia maji tia maji anataka apate pesa ndio atoe pesa kwa hiyo tuliona hakuwa serious bali alikuwa anatuchora tu. hivyo naomba mbia/mshiriki mwenye nia ya dhati kweli hii sisi ni kazi ya maisha yetu tunapenda pia mshiriki wetu afahamu hilo na sio kupotezeana muda.
karibuni tulijenge taifa letu pamoja!