Hahaha,mkuu umenichekesha kweli umevyokimbiza madalali.
Lakini kuna mazingira Dalali hakwepeki.
Maana maisha haya unaweza kukuta eneo unalolipita linauzwa na wewe hujui,ila dalali anadata zote hadi za marehem wenye viwanja.
Kuna mazingira jaribu kutumia dalali.
Njia moja ya madalali ni hii hapa,wewe nenda na dalali,msikilize percent yake anayotaka.Halafu peleleza bei ya mashamba maeneo hayo utaijua tu kirahisi.Kisha akikuunganisha na mwenyemali wewe shusha bei to the base.
Kuna eneo brother wangu alienda kununua chanika,ikatokea hali kama hiyo.Ila cha mwanzo alimuuliza dalali chako kiasi gani,dalali akasema kiasi chake,basi yule jamaa alipounganiswa na mwenye mali,alimuambia tu kwamba mie pesa ipo hii sasa unasemaje.
Basi kawaida ya madalali wanatabia ya kumwambia mwenye mali kwamba jamaa namleta anapesa kweli huyo,ili lengo lao kwamba asishushe bei ili kile chao kiwe juu kama walivyopanga.
Sasa ukiwa na msimamo wa bei,basi usifanye haraka,we jifanye kama huna time nacho tena,basi huwezi amini ndani ya wiki moja au mbili watakutafuta kwa kasi kweli.Maana usiombe shida ikajua wapi pesa ipo ndio kwanza shida zinakuja.