Natafuta kazi

Natafuta kazi

Nasakadoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
343
Reaction score
169
KWA YEYOTE ATAKAYEHUSIKA NA ATAKAYEGUSWA AU KUHITAJI.
Nina elimu ya sekondari.
Ninajua kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza.
Nina leseni ya Udreva daraja A,B,D & E.
Nina umri wa Miaka 25 naelekea 26.
Jinsia yangu ni Me.
Nimewahi kusimamia Baa kubwa yenye Ukumbi wa Harusi,Guest House,Yenye kulaza magari,n.k.
Nimewahi kusimamia shell ya mafuta (ila haikuwa sheli kubwa,ni ndogo kiasi chake).
Pia mimi ni Dreva mzuri wa Bajaj na Magari(hasa hasa Auto,au Manual isiyozidi Gia 5)
Nimewahi kuuza Duka la vitu tofauti tofauti,.
Kwa sasa sina ajira ya kunifanya nijisikie nipo ajirani!
yaani nguvu ni kubwa saana kuliko ninachokipata.

So, naomba kwa yeyote anayehitaji mtu,au kama unamjua mtu au kampuni au taasisi fulani inayohitaji mtu wa kufanya kazi hizi
Kuuza Duka la aina yoyote,Dreva,msimamizi wa mradi fulani au Biashara fulani,n.k.… tafadhali NIPO.
ninahitaji kazi,naamini tutaelewana… kunjua moyo wako nione na mimi katika kuona kwako!
Nipo Dsm Mbezi ya Kimara.
Asante
 
Kwa Uzoefu ulionao, ungeanzisha biashara, ukiwa na fortune hata ya laki 2, unaweza fanya bussiness itakayokupa faida 40000 kwa siku...
 
Na hii ndio moja ya faida ya JF......kutoa jukwaa la kujitangaza namna hii kwa wasaka ajira wenzetu.Big up mkuu safi,wale wenye kufahamu pahala penye kumfaa ndugu yetu chonde chonde naomba wasisite kumsaidi.Sema ndugu hiyo heading yako ndo kidogo umetuingiza chaka(maana nimekuja mbio kweli),ila anyway ujumbe umewafikiwa wahusika wenye mioyo ya kusaidia wengine.

Baraka tele kwenu!
 
Kwa Uzoefu ulionao, ungeanzisha biashara, ukiwa na fortune hata ya laki 2, unaweza fanya bussiness itakayokupa faida 40000 kwa siku...

Ni sawa lakini it need a Capital…
 
Na hii ndio moja ya faida ya JF......kutoa jukwaa la kujitangaza namna hii kwa wasaka ajira wenzetu.Big up mkuu safi,wale wenye kufahamu pahala penye kumfaa ndugu yetu chonde chonde naomba wasisite kumsaidi.Sema ndugu hiyo heading yako ndo kidogo umetuingiza chaka(maana nimekuja mbio kweli),ila anyway ujumbe umewafikiwa wahusika wenye mioyo ya kusaidia wengine.

Baraka tele kwenu!

Mkuu… weupe wanasema "first impression then expression"… bila kutengeneza heading ya maana mtu haufungui uzi
 
Habari Wadau,Members na Non-Members of JF…
Ni juzi kati tu nilitoka kuweka uzi wa kuomba ushauri au msaada wa kile nilichokieleza.

Baadhi walinishauri pale wengine wakaponda ombi langu ila yote heri tu. Tena nilionana na mwana Jf maeneo ya Ubungo anatumia jina la #Mjasiliamali_Elimu humu, alinipa ushauri wa Mawazo mazuri tuu kilichobaki ni utekelezaji.

Sasa Issue ni kwamba (kwa wale ambao labda hawakuona uzi wangu) nimehangaika saana saana kutafuta ajira au kibarua chenye tija,nimeshindwa,nimehangaika pia kujiajiri lakini sikuwa na mtaji wa kutosha kwa hilo. Ndo nikaja humu Jf kuomba msaada wa kimoja wapo au vyote viwili, bado sijafanikiwa labda nimefanikiwa kwa 40%(kwa msaada wa mawazo).

Sasa hivi nilikuwa na Plan hii, na nakuomba msomaji wa Uzi huu ukonsetreiti hapa;
Ukweli kupata ajira ni ngumu saana… na kujiajiri pia ni ngumu kama huna vyanzo vya uhakika vya mtaji.

Mimi nilikuwa naomba kwa yeyote aliye tayari kunifadhili Bajaj (TVS King) au Noah,naomba tuongee…

Unanipa Bajaj halafu mimi nakuwa nakutafutia hesabu…
Kwa hesabu ya haraka haraka Bajaji kwa siku nitakuwa naleta Tsh10,000 hadi Tsh 15,000 kutegemea na Mazingira ya Kazi.
bahati nzuri nimewahi kuwa dreva bajaji so nina experience na hii shughuli.
Tsh10,000×6 (siku)=60,000/-
Hapo Masuala ya Service ni juu yangu.
Au
Tsh15,000×6(siku)=90,000/-
Hapa Service ni juu ya Bosi.
na Service ya Bajaj kama Dreva ni mzuri inaweza kufanyika mara moja kwa Mwezi au kila baada ya miezi miwili
kwa sababu issue kubwa kwenye Bajaj Slider na Hubcup zake ndo mara nyingi husumbua…

Siku ya 7 nimeitoa kwa sababu binafsi ni mkristo so ningeomba niwe nahudhuria Church na kufanya usafi kidogo ndiyo maana nimepiga mahesabu ya Siku sita sita.

Kwa Upande wa Noah huko Pia ni Maelewano tu,maana kuna maeneo yanakuwa na Abiria wengi na hayana lami… so kwangu mimi location nzuri naijua au itategemea na masharti ya mwenye chombo kujua nimletee hesabu sh ngapi baada ya Makato yoote ya siku.

Nadhani mpaka hapo kuhusu vyombo hivyo nimefafanua vizuri kiasi ambacho mwenye chombo anaweza kunitathimini ili tuonane na kupeana majukumu rasmi.
Nina uhitaji kweli,
Leseni ya Udreva ninayo,ina Madaraja A,B,C,D,& E.
Jinsia yangu ni ME umri wangu hauzidi miaka 27.

Lakini pia la Nyongeza sasa labda huko kote nimefeli,
Mimi pia napenda kuuza Dukani,duka lolote lile,liwe la Hardware,Soft Drinks,Casual Wears,Electronics, la Mchanganyiko wa Bidhaa mimi nipo vizuri,ni suala la kuelekezwa siku moja mbili,then We go.
So kama kuna mtu ana una mtu anatafuta mtu wa hivyo naomba tuwasiliane ndugu zangu.
Pia kuna wale Wanaotafuta Madreva wa kuwa wanawapeleka kazini na kwenye Project mbali mbali,mimi nipo Tayari kuwa Dreva wako… tuwasiliane pia.
Kwa kifupi ni hayo tu,naomba mnifikirie kijana wenu,mwanenu,ndugu yenu,n.k.
Unaweza kuni PM au namba yangu ya Simu ni
+255 718 65 11 74.

NITASHUKURU OMBI LANGU LIKIKUBALIWA.
IN GOD/ALLAH WE TRUST.
 
pole ndugu yangu, kwa upande huo, mi binafsi sina msaada, ila ungekuwa umesoma mascom, au haya ya utangazaji haya, kuna redio mpya imeanzishwa maeneo ya kinondoni, so na kuna jamaa yangu pale kala shavu, ningekuconnect, huenda mungu angesaidia, ila kwa upande wako huo, namuomba mungu asaidie wadau wakusaidie.
 
Pole sana ndugu yangu, kwa jinsi ulivyojieleza, nimejikuta nabubujikwa na huruma. Mbali na udreva, fani yako nyingine uliyosomea niipi?
 
usikate tamaa, do struggle,bado una muda mrefu wa kupigana
 
Kijana NASAKADOO umejieleza kwa kirefu na vizuri sana na Mungu atakusaidia.
 
Uckate tamaa ila badili mtazamo na punguza kulalamika then swala la service ya bajaji upo wrong kwasababu watengenezaji hua wanaagiza service kwa kilometers kwanini unasema kwa mwezi? Ajira zipo komaa Ku aply lakini kubwa kuliko yote ni kuzunguka magodauni kila siku kampuni ni nyingi saana zinafungua viwanda na miradi. asante
 
Peleka maombi yako ktk anuani hii:

Mkurugenzi rasilimali watu ,
Shirika la usafiri DSM ltd,
SLP 872. DSM.

Ambatanisha:-
.barua za wazamini watatu waandike kwa mono.
.
.paspot mbili zaki na kila mzamini.

Kumbuka unatakiwa kurejesha 205000/=
 
Kuna nafasi za kazi ya udereva maeneo ya azam icd,mbozi road kazi zipo zunguka kwenye viwanda na si kulalamika hovyo mtoto wa kiume lesen yako nzuri kama na cheti unacho kazi zipo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nani uwezo wa kufanya kazi yoyote halali… Kuuza duka,kusimamia miradi,n.k.
Nishapost saana humu maombi ya kazi… lakini naishiwa kupewa pole na kutiwa moyo! Nimejieleza vya kutosha! Ila naona bahati haijaja kwangu…
Ndo naufungua mwaka sasa…
mimi ni ME… nipo dsm
Nipo tayari kufanya kazi eneo lolote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom