Natafuta kazi, yeyote utakaeguswa Mungu akubariki

PierreLiquid

JF-Expert Member
Oct 16, 2019
596
2,279
Habari ndugu zangu,

mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 Me ninaishi Dar es salaam, nina stashahada ya ugavi ya chuo cha biashara. Ni muda nimeangaika na ajira mpaka ilifika hatua nikaamua kujiajiri kuanzia 1, nimefanya biashara Soko langu kuu likiwa online, ila nimeaanguka mara kwa mara na nikashindwa kusimama tena na yote ni kulingana na kipato nachowekeza kuwa kidogo sana kuhimili hasara.

Toauti na elimu yangu nina uzoefu wa mwaka mmoja kwenye mikopo kama loan officer individual & groups loans.
Monitoring
Disbusment
Collection
Follow ups
Recovery

Siku zote kwenye maaisha yangu namuomba mungu aniletee mtu wa kunipa nafasi ili nionyeshe. Mimi ni muaminifu sana, najituma sana. Ila kitu nafasi ya kunifanya nionekana ni jambo nalolikosa siku zote.

Nahitaji kusimama tena mimi, nahitaji wa kunipa nafasi, naamini huu sio muda wa kuchagua. Wanadamu tunachagua ila Mungu anajua wapi ni sahihi kutuweka.

Asanteni kwa yoyote utakae guswa usisite kuwasiliana na mimi na Mungu atakubariki zaidi.
 
Naona siku chache zijazo ukipata Kazi...jichunge usifanye dhambi ya Aina yeyote ile kwa.wiki.hizi mbili..ukipata Kazi usisahau shukran kwa mungu wako na aliyekupa hiyo Kazi.
 
Naona siku chache zijazo ukipata Kazi...jichunge usifanye dhambi ya Aina yeyote ile kwa.wiki.hizi mbili..ukipata Kazi usisahau shukran kwa mungu wako na aliyekupa hiyo Kazi.
😂😂😂 Sisi watu bhana
 
Back
Top Bottom