Natafuta kazi yeyote halali

Natafuta kazi yeyote halali

Crystal123

New Member
Joined
Mar 1, 2022
Posts
3
Reaction score
2
Mimi ni msichana wa kitanzania, umri wa miaka 27. Nina shahada ya kwanza ya mambo ya kibenki na huduma za kifedha ( Bachelor in banking and finance) kutoka Institute of Finance Management (IFM).

Nahitaji kazi yeyote halali iwe kulingana na Proffessional yangu au kazi yeyote ijayo fundi Shuka ili niweze kuifanya kwa ufasaha na kuongeza tija kwenye taasis, kampuni,bank au sehemu yeyote nitakayokua nafanyia kazi hiyo.

Nina ujuzi wa kutuma comtuper vizuri (Ms word, excel) . Na uwezo wa kuongea kingereza na kiswahili kwa ufasaha.

Nishawahi kufanya kazi mahala fulani kama mhasibu msaidizi , hivyo nina ujuzi wa kazi za kihasibu.Pia nimekua nikijitolea(Intern) katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa muda wa miaka miwili. Naweza kuwa added advantage kubwa katika kampuni au shirika litakalo niajiri , Kwa uzoefu wangu wa miaka miwili ya internship nitatoa support yakutosha katika maswala yote yanayohusiana mapato, kodi(taxes) , e-filling issues ……etc etc


Ahsanteni
 
Kazi zilizotangazwa na utumishi za tra uliomba??
 
mama kaleta kazi kutoka uarabuni hujasikia
 
Ndio mkuu, Ila portal imegoma
Wameniandikia “ lacks relevant bachelor degree as per advert”
Mbona degree yako inaendana Wapuuzi hawa wanapunguza watu ili mradi

Mimi nime apply na Bsc forestry imekubali [emoji1787]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom