Natafuta Kazi/Volunteer

Natafuta Kazi/Volunteer

LillianBucho

New Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
4
Reaction score
0
Nina masters ya community development na project management natafuta kazi/volunteering nisaidieni. Niko tayari kufanya kazi popote. Niligraduate mwaka jana mwezi 11. Help...!
 
Kuna kaz ya uwakala wa Togo,voda,airtell office iko kariakoo kama unahitaji weka number nikutafute
 
Asante sana skidemout nilikuwa namaanisha popote tanzania sio nje ya tanzania. Thanks again.
 
DUH ajira ngumu aisee, kumbe na wenye masterz mnasota, kiasi kutamani kuvolunteer, wengine wameitwa uwanja wa taifa 10840 kwa nafasi 70, karibu benk ya posta uwe freelencer mshahara 140000, ukizembea unakula 50000 kwa mwezi.
 
Asante sana skidemout nilikuwa namaanisha popote tanzania sio nje ya tanzania. Thanks again.

Umemuelewa vibaya. Kasema uwakala wa Tigo. Mtandao wa simu. Alivyoandika Togo ile ni typping error. Si unajua smartphones za qwerty keyboard, herufi "i" na "o" zipo karibu? Haya muelewe tena kisha mcheki PM.
 
masters masters...rudi chuo kaombe ufundishe ata kwa kujitolea, ila nakuonea huruma ila nakutamanii ila sio ishu komaa
 
Hadi wa masters kazi ni ngumu?Kweli hii nchi yetu ni balaaa
 
Nina masters ya community development na project management natafuta kazi/volunteering nisaidieni. Niko tayari kufanya kazi popote. Niligraduate mwaka jana mwezi 11. Help...!

Kama ni ya Mzumbe napata wasi wasi na wewe....Ya Tengeru CDTI iko fine. Sasa sijui wale kama wana Masters.
 
Kua na Masters sio kwamba ndo unaweza pata ajira! Kuna kijana kasoma MBA,kapiga CPA tena single sitting wahasibu mnaelewa namanisha nini,alimaliza MBA yake 2010,kasota kitaa,kafundisha sana kwenye hizi review class centre,mwaka jana ndo kapata kazi PSPF!! Anavyowahi sasa kwenda job!
 
Kitu kumi yuko mlangoni. Kazi hizi jamani
 
ingia zoomtanzania VSO wametangaza post za volunteer unguja,kagera,kilimanjaro na mbeya.......
 
Back
Top Bottom