Natafuta kazi katika field za IT, Accounting na HRM

LastChance

Member
Mar 16, 2020
24
11
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kiume na ninaishi Dar es Salaam, nina Degree ya kwanza katika IT (Bachelor Of Science in Information Technology).

Natafuta kazi katika field zifuatazo, IT, Accounting na HRM.

Waweza ona ni fields tatu tofauti ila hii inatokana na mimi kuwa na experience ya kutosha kwenye fields hizo zote, mimi kwa kifupi ni programmer niliyejikita zaidi upande wa kutengeneza software za Accounting na Payroll japo pia nina tenegeneza other custom software.

Pia nina uwezo wa kufanya kazi katika nyanja nyingine tofauti kama nitafundishwa (mimi ni fast learner).

Pamoja na hayo yote pia naweza fanya kazi kama consultant na Trainer kwenye hizo fields.

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu, nilishawaza hilo changamoto ni kuwa kuna free simple akaunt app nyingi sana. Ila nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu.
Wakati ukiendelea kutafuta kibarua,Tengeneza simple akaunt apps lenga wafanya wadogo wadogo hasa nchi za nje,

kwenye apps unaweza weka paid feature au kui-monetize app, inachukua muda kunufaika nayo ila mvumilivu hula mbivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unauzoefu wa kutengeneza software alafu unatafuta kazi idara ya uhasibu, unataka uache kutengeneza software uende kujifunza kupost and kufile payment vouchers?

unajielewa kweli wewe?
 
Unauzoefu wa kutengeneza software alafu unatafuta kazi idara ya uhasibu, unataka uache kutengeneza software uende kujifunza kupost and kufile payment vouchers?

unajielewa kweli wewe?
Mkuu kutengeneza software siwezi kuacha hata kama nikiwa nafanya kazi yoyote ile, mana kutengeneza software au software engineering ni passion yangu. Sema kwa sasa soko kazi zimepungua sana, zimebaki kazi za kukodishwa online na kufanya module moja au mbili then unalipwa na inaishia hapo.
Nashukuru sana JF kwani nimeweza kupata project kupitia huu uzi. Asanteni sana na kama kuna mtu mwingine wa kunila project au kazi ntashukuru pia.
Asanten

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama una kazi au connection inayoweza mpatika kazi masidie.
Dirisha zuri hili hapa kama hupati kazi jaribu freelancing kama huwezi bid kila project yaani mvivu kama mimi jaribu site za kutundika ujuzi kama fiverr na zinazoendana na fiverr otherwise jaribu kuchukua script GitHub ambayo haikukamilika kisha kamilisha then itupie codecanyon au tengeneza ya kwako ni swala la muda tu.
Mara nyingi ukiona hupati kazi unayopenda jaribu mbadala sikukatishi tamaa. Kazi njema
 
Back
Top Bottom