Natafuta kazi, hii ndio CV yangu

Natafuta kazi, hii ndio CV yangu

mtanzalendo

Member
Joined
Aug 29, 2014
Posts
74
Reaction score
121
Ndugu zangu, mimi mbele yenu ni kijana wa miaka 31 najitokeza mbele yenu kupata msaada wa ushauri au connection.

Mimi ni mwalimu by profession ,nimefundisha kwa miaka 7 sasa .

Nina degree ya education na masters ya public administration .

Nimefundisha secondary na primary.

Naomba mnisaidie ni jinsi gani maweza kuama hii fani ya ualimu.

Uzoefu wangu wa kazi

Mwalimu wa secondary miaka mitatu. ( academic master)
Mwalimu wa primary - english medium miaka 4 ( head of department & principal )

Regional research supervisor mwezi mmoja - survey ya muhimbili university

Sababu za kuama ualimu.

1. Nimeitumikia vya kutosha kazi hii nataka nipate uzoefu mpya.

2. Maslahi ya hii kazi ni madogo mno kiasi kwamba miaka saba kwenye kazi nimejifanyia tathmini sioni hatua yoyote ya maana niliyopiga. Maisha yangu wakati naanza kazi na sasa hayana tofauti nachokipata ni hand to mouth. Majukumu yamekuwa mengi mno sina budi kusonga mbele .

3. Nataka kubadilisha kazi, nimefanya juhudi kwa kujinyima nikasoma masters ya fani tofauti japo mpaka sasa sijapata mrejesho mzuri naamini ndugu zangu mtanisaidia.

Uwezo wangu wa kazi.

Ninaweza kusimama na kufundisha mbele za watu, kuandaa somo na kupima matokeo.

Ninauwezo wa usimamizi wa mradi,ofisi au majukumu yoyote.

Ninauwezo wa kutumia computer programs kama ms word, excel,power point .

Nina uwezo wa kubuni miradi, kuandika mradi na kuusimamia.

Ninafahamu labour law.

Mimi ni muaminifu, muadilifu na mchapa kazi napofanya kazi naifanya haswa.

So naomba sana ndugu zanguni mnisaidie kupata kazi yoyote nje ya fani ya ualimu wa shuleni. Nipo tayari kuanza upya kama trainee au volunteer ilo halina shaka . Nipo tayari kwa kazi yoyote haijalishi elimu yangu wala experience.

Mpaka nimekuja hapa mbele yenu nimezunguka sana karibu ofisi zote Dsm bila mafanikio ata kuvolunteer. Uwezo wangu wa kibinadamu wa kufikiri umefika mwisho.

Naomba ataesoma hapa aguswe na kutoa msaada kwa kadri ya uwezo wake na Mungu atamlipa mara nyingi zaidi.

Kwa mawasiliano .

Unaweza kuniPm

au kunicheki kwa email mzalendo255@gmail.com

mzalendo255 at gmail.com
 
Unaweza kubuni mradi na kusimamia?
frankly speaking, kazi ni ngumu labda tumia mshahara wako kuanzisha mradi wowote ili upate kipato kikubwa .
 
Kama unaweza kuandika proposal nzuri nitafute,nina idea nzuri tukiweza kuimplement tunawezapata financial support kutoka taasisi zetu za kifedha.
 
Unaweza kubuni mradi na kusimamia?
frankly speaking, kazi ni ngumu labda tumia mshahara wako kuanzisha mradi wowote ili upate kipato kikubwa .

Mkuu nna hamu sana ya kuanzisha mradi. Hapa nilipo nina idea ya kuanzisha day care au shule na nna uhakika itafanikiwa sana maana nimetumika sana kuwafanyia wengine wakafanikiwa.

Tatizo ni capital mkuu, yani mshahara nnaopata as mwalimu ni aibu ata kuutaja na wote unaishia kwenye matumizi ya lazima kwangu na family ata kusave inakuwa ishu. Ndio maana naona nikipata kazi nyingine yenye angalau mshahara wa kuridhisha naweza kuanza kujipanga taratibu .
 
Nimekuwa mwl.kwa miaka isiyopungua 9 kwa muda wote huo nilikuwa nataka kubadilisha kazi kama wewe.nilifanikiwa mara 3 na sasa niko nafanya kazi siyo kama mwalimu.

Changamoto ni nyingi lakini nima siri ya mafanikio yako.

Kuna mambo mengi lakini kubwa nililoligundua ni "job interview skills" hili ni tatizo la wengi hata wale ambao hawako katika ualimu lakini pia wanahitaji kubadilisha kazi au kuongezewa mshahara lakini wasijue nini cha kufanya.

Nimewasaidia vijana wengi kuhusu masuala hayo.nina uzoefu wa miaka 10.

Kama utahitaji basi ni pm ili tuweze kupanga appointment ili nawe uweze kubadilisha kazi kadri upendavyo.
Kila la kheri.
 
Shukrani, nakuPM .

Japo ata kuitwa interview imekuwa tabu.
 
Ungegombea ubunge ndugu yangu, kazi ni ngumu sana....Mungu akubariki upate kazi
 
Anzisha ata vile vishule vya kutunzia watoto maana hakuna namna. Kazi ngumu sana wenye kazi zao awataki kuwapa wenzao nafasi ni mwendo wa kubaniana tu.
 
Sasa mtu una kazi afu bado unajiliza hvyo,na wasio na kazi kabisa wasemaje sasa?
 
Kilio cha wengi, ila kumbuka kuwa "knowledge is power".
 
Nenda bank kakope pesa kwa udhamini wa Kaz yako kisha fanya biashara ya hiyo shule unayotaka kufungua,fungua biashara ya stationary, mikahawa ya kisasa,vituo vya kuonesha michi za ligi za ulaya,Kuna miradi mingi unaweza kufanya ili kukuza kipato chako kama Mwalimu.Sio lazima ubadirishe kazi,siku zote huwez kuwa tajiri kama hufanyi biashara hakuna kazi ya kuajiriwa inayoweza kukufanya uwe tajiri labda uingie kwenye siasa,matajiri wote duniani ni wafanyabiashara sio wafanyakazi za ofisin
 
pole mkuu! ila kuna ushauri mdau kautoa apo juu..kasema matajiri wote duniani ni wafanya biashara.........ila nako kufanya biashara kuna hitaji ujuzi aiseee...acha kazi fanya biashara ndo utajua namaaanisha nin:hand:
 
Kama ungekua unaishi maeneo ya mikoani naamin kwakiasi fulan tayari ungefanikiwa kubadilisha fani ama kupanda juu kidogo bt mjini hasa km dar ni mtihani ndugu wasomi wengi wapo ndo maana kwa mtu anayependa mafanikio ni bora akaanzia maisha mikoani
 
Mkuu nna hamu sana ya kuanzisha mradi. Hapa nilipo nina idea ya kuanzisha day care au shule na nna uhakika itafanikiwa sana maana nimetumika sana kuwafanyia wengine wakafanikiwa.

Tatizo ni capital mkuu, yani mshahara nnaopata as mwalimu ni aibu ata kuutaja na wote unaishia kwenye matumizi ya lazima kwangu na family ata kusave inakuwa ishu. Ndio maana naona nikipata kazi nyingine yenye angalau mshahara wa kuridhisha naweza kuanza kujipanga taratibu .

N TGS D mbna mkubwa au una bet na kuhonga malaya
 
Anzisha ata vile vishule vya kutunzia watoto maana hakuna namna. Kazi ngumu sana wenye kazi zao awataki kuwapa wenzao nafasi ni mwendo wa kubaniana tu.

Asante kwa ushauri. napenda sana kuinvest ila tatizo mtaji.
 
Mkuu nna hamu sana ya kuanzisha mradi. Hapa nilipo nina idea ya kuanzisha day care au shule na nna uhakika itafanikiwa sana maana nimetumika sana kuwafanyia wengine wakafanikiwa.

Tatizo ni capital mkuu, yani mshahara nnaopata as mwalimu ni aibu ata kuutaja na wote unaishia kwenye matumizi ya lazima kwangu na family ata kusave inakuwa ishu. Ndio maana naona nikipata kazi nyingine yenye angalau mshahara wa kuridhisha naweza kuanza kujipanga taratibu .
Ulisema umechoka kufundisha.. Sasa hiyo day care na shule si zitakuboa tu?
 
Back
Top Bottom