Nipo hapa, njoo! Au sema upo University gani? Maeneo yapi? Unasoma kozi gani? Mwaka wa ngapi? GPA yako ya hivi karibuni ni ngapi? Kwenu wapi? Wewe kabila gani? Umri wako je? Dini gani? Kwenu wewe ni motto wa ngapi? Wazazi wako wapo? Ulilelewa na Wazazi wako wote, mmoja au hakuna? Wewe ni mrefu, mfupi au wa wastani? Ni maji ya kunde, mweusi, mweupe au mwekundu? Umewahi kuwa na mpenzi? Kama ni ndiyo, ilikuwaje mkaachana? Kama siyo, kwa nini? Na kwanini leo, tena muda huu ndipo ulipoamua kutafuta Girlfriend? Kwanini isiwe juzi, jana au kesho? Hivi nini tofauti ya Girlfriend, mchumba, mpenzi na demu? Unayaelewa vema majukumu yako pindi utakapompata huyo unayemuita Girlfriend? Nini mipango yako katika maisha, hasa baada ya kumpata huyo Girlfriend? Umeshawaambia na Wazazi wako kuwa sasa unasaka Girlfriend? Nani mdhamini wako hasa katika hatua hii uliyofikia? Naomba unijibu haya kasha tukutane!