Natafuta fundi wa computer dsm

mshamu

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
418
Reaction score
134
Za wakati huu wana JF mimi nipo kibaha nina computer mbili aina ya Dell zinatatizo la kushindwa kuwaka zinawaka taa ya njano tu na siyo green kama zingine. Jamaa wa karibu wanasema ni mother board sasa naweza kupata fundi wa kunisaidia kwa hili naweza kuja nazo ofisini.
 
Angalia usije ibiwa vi mashine vyako ..mafundi wako kibao..chakufanya...kawaulize mafundi wa mtaani kwako..then wao ndo warakupa rufaa ya kuwaona wakongwe..au kama unajua company profile ya center yeyote ambayo wanatengeza..itz ok wafuate...

Nb.kuwa makini na madalali wa online wengine wezi..
 
mtafute jamaa yangu anaitwa fred yupo pande za sinza kijiweni, mcheki kwenye namba 0712228405
 
Rafiki
Naweza kukusaidia nipatie model number ua hizo Dell zako. na je inawaka njano wakati gani?
Naomba ufanye yafuatayo. toa battery ya laptop halafu weka umeme uwashe. je ni taa ya rangi gani inawaka?
weka battery toa umeme ni taa ya rangi gani inawaka. ninaweza kuksaidia bila hata kuja kwako
Nasubiri majibu yako
 
Shida ipo kwenye kiwango cha umeme kinachoingia ktk mashine. Inawezekana tatizo likawa katika adaptors au ndo power supply part ya motherboard ya mashine.
 

Nipo makini ndugu najua mafundi feki na wengi bila kuwa na ofisi sikupi kazi yangu
 

Samahini kwa kuchelewa kuwajibu aina ni dell desktop na siyo laptop optiplex 745 na 520 huwa inawaka wakati tu wa kuwasha na inabaki hivyo hivyo. Nashukuru kwa nia yako ya kunisaidia
 
Shida ipo kwenye kiwango cha umeme kinachoingia ktk mashine. Inawezekana tatizo likawa katika adaptors au ndo power supply part ya motherboard ya mashine.

Inawezekana kaka kwa kuwa wengi wanasema na motherboard sasa inawezekana nihizo adaptor
 

Yangu aina ya RM(Research Machines) ina-blink taa zake alaf feni inazunguka for 5 seconds then......nothing.What's the problem?Someone told me ya kuwa ni motherboard.Could someone direct me to a COMPETENT electrician?????Natanguliza shukran.
 
1.Ofisi na kazi 1
Mie nadhani watu wenye matatizo wengi humu hawako serious kwa kuwa wanataka mteremko sana,Vile kwa kuwa
Watanzanziba tunapenda sana mteremko basi ukimwambia mtu aje ofisini kwako kusikia "ofisi" tuu anajua anakwenda
kukamuliwa pesa badala yake anasubiri wadau kwenye uzi kama huu kutoa solution.Mie naona njema kabisa kufa kufaana.

2. Ofisi na Kazi
Kumekuwa na mafundi version ya internet(google) nao nawaamini sana maana ni kipaji hadi kufikia hatua ya ku-google na kupata solution ya tatizo lakini wasisahau wale wenye experience zao miaka 10 kwenye game unadhani charge ya service ya fundi wa miaka 10 na version ya google itakuwa sawa?

Kwa experience yangu ya vijimiaka kadhaa kwa issue ya Dell Optiplex GX 520 - 755 kwa 97% ikiwaka orange ujue motherboard iko na shida. Kupata mpya inakwenda kuanzia 150,000 kutegemea na duka hadi 200,000 kwa used inaaanzia 80,000/=

Nawakilisha

Askyade (The Agent)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…