Natafuta ajira, nina elimu ya kidato cha nne

Natafuta ajira, nina elimu ya kidato cha nne

wonder6

New Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
3
Reaction score
0
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi ni kijana wa umri wa miaka 22, nimemaliza elimu yangu ya form four mwaka 2010 na sikuwa na matokeo mazuri sana pia sikubahatika kusoma kozi yeyote ile mpaka sasa ni mwaka wa nne, sina ajira na maisha yangu yamekuwa ni magumu sana. Naombeni msada wa ajira, hakika niko radhi kufanya kazi yeyote ile.

Mungu awabariki sana
 
I can feel what you are going through. Wish I could be of assistance. Mungu akutangulie
 
Pole mkuu ila hapo mwishoni kabisa ungepaondoa au rekebisha!!!!

* hakika nipo radhii kufanya kazi yeyote ile *

Dunia imeisha saivi kuna kazi zina laana!!!
Ni hayo tuu!!!
 
Pole mkuu ila hapo mwishoni kabisa ungepaondoa au rekebisha!!!!

* hakika nipo radhii kufanya kazi yeyote ile *

Dunia imeisha saivi kuna kazi zina laana!!!
Ni hayo tuu!!!

nashkur mkuu
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi ni kijana wa umri wa miaka 22, nimemaliza elimu yangu ya form four mwaka 2010 na sikuwa na matokeo mazuri sana pia sikubahatika kusoma kozi yeyote ile mpaka sasa ni mwaka wa nne, sina ajira na maisha yangu yamekuwa ni magumu sana. Naombeni msada wa ajira, hakika niko radhi kufanya kazi yeyote ile.

Mungu awabariki sana

mimi nimemaliza chuo 2009,sasa nimejiajiri na naendesha maisha yangu vizuri,nakushahuri kijana usisubiri kuajiriwa fursa zipo ,jiajiri mwenyewe.
 
Muite basi ndugu yangu umuonyeshe njia ulitumia,si ndio anachoomba. Muokoe!
mimi nimemaliza chuo 2009,sasa nimejiajiri na naendesha maisha yangu vizuri,nakushahuri kijana usisubiri kuajiriwa fursa zipo ,jiajiri mwenyewe.
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu mimi ni kijana wa umri wa miaka 22, nimemaliza elimu yangu ya form four mwaka 2010 na sikuwa na matokeo mazuri sana pia sikubahatika kusoma kozi yeyote ile mpaka sasa ni mwaka wa nne, sina ajira na maisha yangu yamekuwa ni magumu sana. Naombeni msada wa ajira, hakika niko radhi kufanya kazi yeyote ile.

Mungu awabariki sana

Nilimaliza sekondari mwaka huo huo na hakuwepo wa kunipeleka mbele zaidi ya hapo. Ila had leo hii, tayari nina professions kama 5 hivi. Yaani naweza kuajiriwa na kuishi kama Graphics designer, Web designer, Video editor au Motion graphics artist, au mwanamuziki (guitarist, pianist, muimbaji)

Kuwa na kipaji na kukifuata pia inachangia, ukikitumia kinafungua milango mingine (hili limethibishwa na Biblia pia, kitabu cha Methali). Lakini pia wepesi wa kujifunza na kujisomea vitabu vingi (hii inakupa inspiration na msukumo wa ubunifu).

Moja ya kitabu nilichowahi kusoma na kilinitoa (kasi ya mafanikio iliongezeka) kinaitwa "How to get whatever you want". Humo ni kanuni moja tu ndo inachambuliwa: ASK. yaani omba, mfate mtu...mweleze tatizo, mwangalie machoni...onesha unahitaji. sio wote watakataa.

Makanisa pia yalinisaidia sana, nikakutana na watu walioni inspire kufatilia skills ambazo nimezitaja hapo juu. (Note: ni kwasababu nilikuwa najua kupiga kinanda/gitaa hivyo walinipokea bila shida).

Research kwenye mtandao pia ilinisaidia sana (Google, Youtube na EHow.), Mafunzo kwa kusoma articles na kuangalia videos mengi yalitoka hapa. Baada ya hapo nikaenda chuo ku certify knowlwdges zangu.

Point yangu: Ni ww mwenyewe ndo utakae jiletea mabadiliko. Usijihurumie, fight hadi kieleweke or die trying. Jishughulishe kwa chichite kinachoweza kupatikana sasahivi lakini bila ujuzi wa maana utaishia kushika mia mbili mia mbili tu. Kwahyo piga vibarua huku unasoma. ungekuwa Arusha, ningejitolea kukupa tution ya Graphic design halafu unune mtihani chuo kwaajili ya cheti
 
Back
Top Bottom