Nasumbuliwa na msuli wa mguu wa kulia, naombeni msaada wenu wa kitaalam

Tatemahunda

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
232
91
Wakuu poleni na majukumu,
ni wiki ya pili sasa nasumbuliwa na msuli wa mguu wa kulia, mwanzoni mguu ulianza kuvimba kuanzia magotini hadi chini ila haukua na maumivu, ila kila nilipojaribu kutembea kidogo nilikua nikihisi kama msuli unauma kwa mbaali sana, nilipoenda hospital nikaandikiwa dawa tofauti 3, diclopa gel, Neuro support na vitamin., nilipoanza kutumia tu madawa haya sikuchukua muda sana maumivu ndio yakaanza, saiz maeneo ya chini uvimbe umepungua kabisaa, ila maeneo ya kwenye paja ndio panauma sana, wakati mwingine usingizi hauji usiku kwa maumivu, halavu maeneo ambayo panamaumivu panakua pagum sana, nashindwa kurudi tena hospitali kwakua dokta alisema hadi nimalize doz ndio niende, dozi yenyewe ni mwezi mzima .,naomba kuwasilisha!
 
Una uhakika ni msuli?

Unajua msuli ni nini kwanza?

Kwa kufuata hayo maelezo yako inaelekea una tatizo jingine tofauti kabisa na la msuli.

Jifunze kwanza msuli/ misuli ni nini.
 
ongeza na hii mkuu inaweza kua msaada kwa maumivu ya misuli
AMITRYPTINE TAB KIDONGE KIMOJA USIKU KWA WIKI MBILI
 
Una uhakika ni msuli?

Unajua msuli ni nini kwanza?

Kwa kufuata hayo maelezo yako inaelekea una tatizo jingine tofauti kabisa na la msuli.

Jifunze kwanza msuli/ misuli ni nini.

kiukweli mkuu Mimi nabahatisha tu, mana nilienda hospital dokta akaniandikia dawa nilizotaja hapo juu, kilichonitia wasiwasi docta mwenyewe hata wale manes walikua wanamdharau the way alivyoandika izo dawa, ikabidi wafanye editing kwanza Ndio nikaruhusiwa kwenda pharmacy, alichoniambia dokta ni kwamba kurudi pale ni hadi nimalize dozi, ambayo ni 30 days, sasa nimetumia dawa ni wiki ya pili hii sasa sioni matumaini... naomba kama kuna kitu unafahamu unaribu kunielimisha,ni wiki sasa sizalishi chochote, hata mita 100 siwezi kutembea.
 
Nenda kamwone daktari mwingine.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu! mana mwenyewe nilisha comment kua ni msuli tu kumbe huenda ni tatizo lingine, mana kinachotokea ni kwamba Mara nyingine huleta uvimbe mithili ya jipu, na uvimbe huo unaweza onekana hata sehemu tatu kwenye huu mguu! yaani apa kwenye base ya mguu, kwenye paja na kupita goti chini kidogo, uvimbe huu hua na maumivu makali sana mithili ya jipu, na wakati mwingine hua unahama hamahama usawa huuhuu..
 
Ukienda hosp chek na mgongo pia
 
Na jee huuma zaidi unapokaa kitako kwa muda mrefu?
yani maumivi ni maeneo ya mapajani hasa kwenye 'mtoki ', ila kuanzia kwenye goti kuja hadiw kwenye vidole pamevimba uvimbe ambao hauna maumivu isipokua kwa mbaaali sana...
 
Mkuu daktari asije akakwambia urudi bàada ya mda Fulani bahati mbaya ukazidiwa ukasema mpaka dawa ziishe.

Tafadhali rudi haraka sana hospitali. Dawa nyingi baada ya siku tano utajua tu zina Fanya kazi au la. Nakushauri ukamwone daktari bingwa wa mwili mzima. Nafikiri wanaitwa doctor of internal medicine.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu, ngoja weekend iishe nirudi tena hospitali
 
Back
Top Bottom