Nassari: Sina nia ya kugawa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nassari: Sina nia ya kugawa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 11, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]


  na Waandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), amesema kuwa hana nia wala dhamira ya kuchochea na kuhamasisha mgawanyiko katika nchi kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana, juu ya maneno anayodaiwa kuyatoa Jumamosi kwenye mkutano wa hadhara wa chama chake wakati wa uzinduzi wa operesheni ‘vua gamba vaa gwanda’ kwenye viwanja vya NMC, Nassari alidai lengo la hotuba yake lilikuwa kuhimiza serikali na jeshi la polisi lishughulikie mauaji ya watu na kudai hakulenga kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.

  “Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa; chama changu siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini wala historia, ningependa ifahamike kuwa sina lengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile kama ambavyo imekuwa
  ikitafsiriwa,” alisema Nasari.


  Alisema hata kauli ya ufafanuzi iliyotolewa na Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe, kwenye mkutano huo baada ya yeye kuzungumza iliweka mkazo juu ya msimamo wa CHADEMA wa kuunganisha nguvu ya umma katika maendeleo ya Watanzania.


  “Hata alipohojiwa na vyombo vya usalama kutaka kujua nilimaanisha nini aliwaeleza hivyo,” alisema.


  Nassari ametoa kauli hiyo siku moja baada ya jeshi la polisi kudai linasubiri ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ili waweze kumfikisha mahakamani pamoja Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche, na mwanachama Ally Bananga ambaye alikuwa amehamia CHADEMA siku hiyo ya mkutano akitokea CCM alikokuwa akishika nyadhifa mbalimbali za uongozi.


  Naibu Kamishina wa Polisi, Isaya Mungulu, aliwaeleza waandishi wa habari juzi kuwa baada ya kuwahoji wamebaini makosa wanayowatuhumu nayo yanaangukia katika kifungu cha sheria namba 63 b cha kanuni ya adhabu, sura namba 16 ambapo inahitaji ridhaa ya DPP kabla ya kuyafikisha mahakamani.


  UVCCM wamshukia

  UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kuviwajibisha baadhi ya vyama ambavyo vinatumia vibaya uhuru wake.

  Katibu mkuu wa umoja huo, Martin Shigela, alisema hayo jana alipokutana na wanachama wa umoja huo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akidai kuwa amesikitishwa na kauli iliyotolewa hivi karibuni na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ya kulitaka jeshi la polisi kuwakamata waliohusika na mauaji ya wanachama wake, vinginevyo wangelijitangazia uhuru wao.


  Alidai kuwa kauli ya Nassari ni ya kibaguzi na yenye lengo la kuchochea umwagaji damu, hivyo, lazima hatua zichukuliwe dhidi ya viongozi wa aina hiyo.


  Aliwaambia wanavyuo hao walioandamano kwa ajili ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mabadiliko ya baraza la mawaziri kuwa CCM inalaani kauli hiyo kwani siyo kauli nzuri katika mwenendo wa kisiasa.


  Hata hivyo, wakati Shigela akilalama, tayari viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA, wametoa maelezo kuwa huo sio msimamo wa chama chao, na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, alisimama na kukemea kauli hiyo.


  Kwa upande wake, Nasari amedai kuwa kauli yake haikuwa na lengo baya na ililenga kuweka mabadiliko ya kihamasa katika mikoa hiyo ili wengine waone wivu wa kimaendeleo kwa mikoa ya kaskazini ambayo inaonyesha mabadiliko makubwa.


  “Mimi ni mtu mdogo tu sina nguvu hata kidogo ya kutangaza uhuru huo wa sehemu yoyote ya nchi” alifafanua Nasari.


  Habari hii imeandaliwa na Danson Kaijage,
  Hamida Ramadhani, Dodoma na Grace Macha, Arusha  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ni kauli ya Mtu Mmoja sio chama cha Chadema, na ameelezea kuwa hana nia hiyo; Wajanja wengi wameichukua hiyo statement na kuiweka kama ni Ubaguzi wa Chama

  Kweli Chama Tawala wana sera? au kila kitu ni lawama?
   
 3. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mungu huwa hawafichi wanafiki, watu walisema chama hiki ni cha kidini wakabisha mungu akawaumbua akaibuka mtei akadai waislam ni wengi katika tume ya katiba. watu wakasema chama hiki ni cha watu wa kaskazini mkabisha matokeo mtoto mdogo nasari akatoboa waliyoongea ktk vikao akaja na hoja ya watu wa wajitenge hayo ndio malengo ya chadema tujihadhari na chama hiki.
   
 4. B

  Bwana Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama ndivyo ulivyomaanisha basi naamini hakuna lugha ngumu kama kiswahili.
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Dogo kachuja kwa kAsi ya ajabu,ila si asamehewe? Nini tatizo?
   
 6. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,929
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  wapeleke darasan hao
  watakuelewa tuh
  mweche macho haambiwi tazama
   
 7. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  sifa zipi zinahitajika kujiunga JF maana hekima iko mno chini hasa kwa magamba na makuwadi wao
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kachuja kwa nani? au stress ndo znawasumbuwa?
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kauli ni ya chama msemaji ni Nassari acha kupindisha maneno mkuu.
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Le totoz,darasa la saba ambaye CV yake kubwa ni kuchunga ng'ombe.
  Kauli ya kwanza kitaifa ni kuua Taifa hapo unategemea nini.

  Na mapimbi wa brain wanamshangilia kana hawna akili nzuri.
  Hakuna dili hapo.
   
 11. Jeni

  Jeni Senior Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nassari ametereza au ameteleza kwa wenye kujua lugha hilo halina ubishi tusipende kutokoselewa. Hakujua impact ya maneno yake na changamoto iliyopo kwa sasa katika siasa na kwa hilo yule anayeona kichaka tu basi haja imempata au kama ni pumu imepata mpumuaji
   
 12. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hivi Lusinde aliyethibitisha kuwa jela kuna kitu Lema alifanyiwa, je? Lema alikubali? kama la, faili la kesi ya jiwehai limesharudi toka kwa DPP? DUO STD, Period!
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  "Kumetokea sintofahamu..." hiki ndicho Kiswahili cha kilimbwende siku hizi au?

  Kiswahili ninachokijua mie kinavutia kwa logic, mbona naona hapa kama tunataka kufuata logic ya juu chini kama ya Kiingereza vile.

  Eti "kumetokea sintofahamu" kama kumetokea sintofahamu umejuaje?
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  mbona hata mkeo kachuja pia?
   
Loading...