NILIPOSOMA HEADING YAKO NILITISHIKA!
Labda nitoe kisa nilichoshuhudia!
Jumamosi nilikuwa kwenye msiba wa ndugu wa MwanaJF mwenzetu katika eneo la Arumeru!
Mara MC akatangaza kuwa kuna salamu za vyama, nikaona kundi kubwa la wanaCDM, wakiwa wamepiga Gwanda, wakasonga mbele kwa machungu mbaya kabisa, na akina mama wakilia, wakasaini daftari la msiba, na kuwasilisha rambirambi yao(fedha) kwa wafiwa...Kisha wakaondoka wakinyanyua mikono, na waombolezaji kwa muda waliacha shughuli ya maombolezo na kufuatilia kwa umakini tukio lile, huku wakipunga mikono kwa nguvu hewani, huku wakizungumza kichinichini kuwa hakika tunaomba uchaguzi uwe kesho! ili magamba wakomeshwe!
Hakika kama kungekuwa na mtu kichaa pale akatamka...Peopleeeeez!, sijui hali ingekuwaje!~
Baada ya tukio hilo MC akaendelea kuita kama kuna chama kingine chochote kilichokuwa na uwakilishi, ambapo hakukuwa na wengineo!