UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,247
- 11,083
Nsikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.
Kwanza kabisa nikiri,mimi ni mpenzi na shabiki mkubwa wa Dar Young Africans au kwa Kiswahili Yanga.
Klabu hii imepitia changamoto sana hasa wakati ambapo wenzetu waliingia kwenye mabadiliko ya kiundeshaji,wakati wao wakiwa kwenye machakato wa mabadiliko tayari walikuwa na mtoa fedha ambaye aliwekeza fedha zake ili kuiletea klabu matokeo chanya,matokeo yake tuliyaona kwa kututesa kwa takribani miaka 4.
Wakati wenzetu wakiwa na furaha kwa misimu minne,sisi wengine tulikuwa tukisuasua kwa ukosefu wa fedha.
Nitoe shukurani sana kwa uongozi wa timu yangu ya Yanga kuingia kwenye mabadiliko ambayo leo tunaona faida yake.Sasa pamoja na kuwa tunaona faida ya kuwa na mfumo wa uendedhaji timu ulio imarika lakini bado nina mashaka makubwa mno na benchi la ufundi.
Nimshukuru Kocha wetu Nasredin Nabi tangu amekuja nchini Yanga imekuwa ikicheza mpira mkubwa mno lakini bado nina mashaka makubwa pia na ufundishaji wa kocha huyu.Yanga hii iliyokamilika kila idara sijui bado inakosea wapi kwani tuna tatizo kubwa la upatikanaji wa mabao.
Nakumbuka miaka mitatu hadi minne iliyopita Yanga ilikuwa inatoa dozi za mabao ya kutosha kwa timu pinzani lakini kwasasa pamoja kuwa na striker bora hapa Afrika lakini tunaambulia magoli machache.
Sijajua ni mbinu za ufundishaji za kocha Nabi au uenda tatizo ni nini!,Kwa Yanga hii iliyokamilika kila Idara nilitegemea tunapoingia uwanjani mpinzani yeyote akikutana na kipigo kidogo basi iwe angalau goli tatu,lakini ushindi wetu umekuwa wa kupambana sana,nafasi tunatenegeneza za kutosha lakini tunapata goli chache!.
Nadhani kwasasa Nabi anapaswa apumzike ili aletwe kocha mwingine mwenye mbinu mpya!.
Nauomba uongozi huu msimu uwe wa Mwisho kwa Kocha Nabi,Nabi ni kocha mzuri sana lakini pia anayo mapungufu yake.
Ni hayo tu.