Nasimama na Spika Ndugai

CAG kama aliona kila anachokipeleka uwe ushauri au maoni aidha kwa serikali au bunge avitekelezwi,alichukua maamuzi gani au kwanini asijiudhuru

Unapotaka kitu ukisemacho kiwe na impact unakizungumzia sehemu ambayo maneno yako yakisikika yatafanikisha yale uliyotaka yatimie; mfano ni huu wa CAG juu ya udhaifu wa bunge, unadhani hayo maneno angerudia kuyasema akiwa nchini yangekuwa na msisimko na impact kama yalivyopata? Sio siri kuwa Ndugai kama Spika ni dhaifu sana na ndio maana bunge nalo ni dhaifu; mambo yanayofanywa na bunge kwa mfano kukamatwa hovyo na kudhalilishwa kwa wabunge yasingeweza kutokea enzi za marehemu Sitta hata Anna Makinda for that matter!! Ndugai ana maradhi yanayomsibu hivyo sidhani kama hata ubongo wake uko salama.
 
Daah umemjibu vizuri sana... Asipokuelewa basi tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda kuna ukweli, maana wasemalo watu sana kuna....Ila hakutakiwa kusema hayo huko Ughaibuni kama vile. Kajisafisha huku analitia bunge letu tukufu matope!
Labda naye alijiona untouchable, labda alijisahau na kujiona bora, uzuri kasoma, atarudi kufundisha Accountancy vyuoni au Auditing mitaani, hatakufa njaa..
 
Mkuu wali ni mzuri sana lakini ukiwekwa kwenye sehemu isiyo sahihi haufai kabisa kwa matumizi.

CAG amekosea sana hata maadili ya kihasibu. Nazani amemiss behave big times inabidi ajirekebishe tu.
Angeweza kufuata taratibu za kihasibu wala haya yote yasingekuwepo. Mhasibu lazima uwe na siri kali sana la sivyo huko kwenye makampuni watu wangekuwa wanalia kila siku. Nazani kuna pressure anapata ambayo anaona haiku sawa angeachia tu ngazi ili awe huru.
 
Nimekuelewa mkuu lakina hata wenye CPA waje hapa watakuambia.. Huwezi sikia Auditors anaongelea mambo ya mteja wake kwenye public. Kama mambo yameenda vibaya basi anatakiwa afuate utaratibu.
 

Kama hamtaki ya nje si bora mtafute dunia yenu mjifungie na kufanya mambo yenu ndani, lakini dunia hii imekuwa Kijiji na mipaka imebaki katika fikra na border post tu. sasa mtu anasema popote na ukweli haubadiliki kwa kutegemea sehemu mtu anayosemea, kikokotoo kimejadiliwa na bunge na wabunge kusema ndioooooooooooo na supika kupitisha sasa nia ya kikokotoo imeonekana baadae kwamba serikali ndio imekopa pesa za mifuko na haitaki kulipa sasa na mzigo wamesukumiziwa wastaafu ili wafe mapema wazurumiwe.

Hili ndio Bunge ambalo limesimamisha shughuli zake kwa muda kumpongeza Jiwe kwa kuamua kununua korosho kwa pesa za Benki na kwenda kuhifadhi katika maghala na wajeda wakiongozwa na CDF kwenda kusomba tena afadhali CAG alisema Dhaifu sie huku mtaani tunaona ni Ujazzband. Kama kasemea nje imekuwa nongwa lini hawa wa awamu hii wamekubali kusemwa humu nchini, Zitto kaitwa mara ngapi kwa kusema tu na Lisu unajua alipo kwa kusemea humu nchini, watu wanasema mpaka wafiche ID kama humu JF na umeona Mero anavyosumbuliwa.
 
Inatosha na imetosha...well said mkuu Chakubanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakubanga nimekuelewa.Hujamzuia CAG kufanya kazi yake, bali asimamie na afuate taratibu sahihi.Kwenye dosari apendekeze cha kufanywa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani nikiamka asubuhi nisilisikie hili dude CAG, yaani liwe limeshaachia ngazi haraka sana.

Sio ukifanikiwa tu kuamka, hata ufie usingizini bado ukweli aliosema CAG uko palepale. Bunge ni dhaifu na hilo liko wazi. Hata wamfukuze kazi huyo CAG bado bunge itabidi lijitafakari kuhusu huu udhaifu aliosema CAG. Sisi wananchi tunaojitambua kila siku tunasema bunge letu ni dhaifu, na CAG amekazia kwa ushahidi. Rais anachotaka pesa bila ruhusa ya bunge, kama bunge sio dhaifu maana yake ni nini? Ni hivi penda usipende bunge ni dhaifu.
 
[
QUOTE="Geniustin, post: 29936439, member: 131613"]Hata kama ananyoosha ukweli, lakini hawezi kuidharirisha Inji popote pale achilia mbali huko ughaibuni.


Tumefundishwa Staha, kuchukuliana, kuheshimiana.
Hata kama kuna shida mahali, tumalizane wenyewe kwa vikao na mijadala ya ndani.

Uzalendo kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]

Staha kwenye wizi? Tuvumiliane kwenye wizi wa 1.5t? Siku hizi ni ngumu kutofautisha uzalendo na ujinga. Huyo CAG akifika kwenye hicho kikao atalionyesha bunge lilivyo dhaifu kwa kutaka wamuonyeshe wapi wamehoji zilipo 1.5t, wasipomuonyesha jibu la udhaifu litakuwa wazi. Isitoshe kwa hili alilosema CAG hata kama watamsumbua ukweli kwa bunge ni dhaifu utaendelea kuwa wazi na sisi wananchi tunaojitambua tutaendelea kulidharau.
 
Uko vizuri bro nimependa ulichoandika... Usikatishwe tamaa na comments ...
Yes Bunge ni dhaifu.... Ila bado ni muhimili usiotakiwa kutukanwa na CAG.....

Uwe dhaifu halafu usitukanwe? Usipotukanwa huo udhaifu utakaa uishe?
 
Yaani umeandika matapishi + uharo next time jipange

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali fikirishi....
Je ni nani kati ya Spika na CAG ni mzalendo....
Naomba Tuanzie hapa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…