Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,505
Hao wanaopewa vitalu vya uwindaji nyama wanapeleka wapi? Maana kuna watu wanasikia toka utotoni kwamba nchi yao ina mbuga nyingi tu zenye wanyama wanaoliwa wa aina zote lakini hajawahi kula hata nyama ya nyati wala swala!!!! Sasa kama hakuna wanyama wanaowindwa hivyo vitalu vinatolewa kwa kazi gani? Kama wanyama wanawindwa kwa ajili ya kitoweo ni kwanini wananchi hawapati fursa ya kufaidika na kufurahia rasilimali zao? Ifike sasa serikali ikafungua mabucha ya nyamapori ili wananchi wajisikie fahari ya kuwa na hufadhi za wanyamapori.