Nasikia kiu mara kwa mara

Acha Dhambi

Senior Member
Oct 19, 2010
145
41
Nina tatizo la kuwa na kiu ya maji mara kwa mara hata nikinywa maji baada ya muda mfupi nasikia kiu tena.

Pia asubuhi nikihamka nasikia kiu sijui ni Dalili za nini mwenye ufahamu anisadie.
 
Nina tatizo la kuwa na kiu ya maji mara kwa mara hata nikinywa maji baada ya muda mfupi nasikia kiu tena pia asubuhi nikihamka nasikia kiu sijui ni Dalila za nini mwenye ufahamu anisadie
Wahi kwa wataalam kapime sukari kwa kawaida kiwango cha sukari mwilini ni 4-7 ikizidi hapo tayari ni tatizo! Wahi hospital
 
Hiyo Ni moja ya Dalili ya Ugonjwa Wa Kisukari,

Dalili nyingine Ni kama,

1.Kukojoa Mara kwa Mara hasa nyakati za usiku.

2.Kuongezeka kwa hamu ya chakula/Njaa.

Fika Hosp Mapema, Mueleze Mtaalamu mambo yote.

Au unaweza ukanunua kwanza mashine ya kupimia Sukari.

Ugua Pole.
 
Pole sana jitahidi umuone daktari akufanyie vipimo mwili ukiwa na mabadiliko yoyote na ukaona ni jambo geni muone daktari
 
nenda kapime sukari mkuu... tena wahi haraka...
Kama ukikosa sukari basi itakuwa labda hauna maji ya kutosha mwilini
 
Wahi kwa wataalam kapime sukari kwa kawaida kiwango cha sukari mwilini ni 4-7 ikizidi hapo tayari ni tatizo! Wahi hospital
Zipo sababu nyingi tu za mtu kupata kiu ya mara kwa mara (polydipsia) kisukari ikiwa ni mojawapo. Dalili hii pekee haitoshi kuamua kwamba mtu anaumwa kisukari kwa hiyo naafiki na waliopendekeza kupimwa ili kupata uhakika. Ni muhimu pia kujua dalili nyingine kama kukojoa mkono mwingi mara kwa mara, kuhisi njaa mara kwa mara na kupata haja kubwa nyingi.
 
Nina tatizo la kuwa na kiu ya maji mara kwa mara hata nikinywa maji baada ya muda mfupi nasikia kiu tena.

Pia asubuhi nikihamka nasikia kiu sijui ni Dalili za nini mwenye ufahamu anisadie.
Pole sana, Usistuke kwanza tupe :- umri wako, Hulka yako (mpole /mkali/mwepesi kupandisha/mvumilivu/nk nk)!1
mengine ...
 
Jamani Wakuu mliotoa kuwa itakuwa ni dalili ya ugonjwa wa Kisukari, je Kisukari kinasababishwa na nini?
 
Pole sana, Usistuke kwanza tupe :- umri wako, Hulka yako (mpole /mkali/mwepesi kupandisha/mvumilivu/nk nk)!1
mengine ...
Pima kisukari
nawashukuru wote kwa ushauri wenu nimepima sina sukari hili tatizo nahisi kama liko kooni kwani wakati mwingine inakua kama kikoozi kizito hivyo kunilazimu kuhitaji kumeza mate mara kwa mara hivyo kunifanya nahiitaji maji
Ushauri wenu bado ni muhimu
 
Ok.. Jeee ushajaribu maji ya mchai chai... unaongezea na juici ya ndimu !! unakunwa kama chai au kahawa !! Basi iwe dafi (warm drink) !!
 
Mara nyingi huwa dalili za ugonjwa wa kisukari unakunyemelea
Hivi hata mtoto mdogo naye anaweza kupata kisukari...!? Kuna rafiki yangu analalamika sana kuwa mwanae mwenye miezi 22 anakunywa maji sana hasa nyakati za usiku. mwanaye huyo na umbo kubwa na uzito wa kg 14. Wako Maeno ya Dar (Mbagala kuu)
 
Mkuu pia nina hili tatizo toka Jana usiku! Nimeamka kama nimenigwa shingo, basi nikanywa maji...! Mpaka saizi, nakunywa maji karibu karibu
 
Back
Top Bottom