Sasa kwanini uhangaike na MTU anayetaka kuharibu ndoa yako tena ni rafiki ya mkeo huyo lengo ni kuharibu hafai kabisa, eti unamuonea huruma, kuna vtu vya kuhurumia ila sio hyo issue, kwanza mkeo hakuamini tena utamfanya aanze kuchepuka bureCariha usiseme mchepuko sina mpango nae wowote huyu dada isipokuwa anatia huruma namna anavyoniomba kumsaidia lakini mimi pia sio mwanaume suruali napambana japo mambo yapo kushoto kidogo kwa sasa
Naunga mkono hoja maana sa hivi ndio yuko sehem salama...Mtafune kwanza ukisha mtafuna utapata akili ya kumsaidia ila usipomtafuna utaendelea kutuomba ushari tu. We mtafune bhana mtoto then mengine yatafuata
Wana jamvi nina mke wangu ambaye ni HR katika kampuni fulani hapa Dar na mimi ni mfanyabiashara japo mambo yangu yameyumba sana kwa sasa hivyo wife ambaye ndio amepata ajira mwaka huu anaboost sana mambo ya familia na next week alipanga tuvute usafiri ili kurahisisha shughuli zetu na pia kumuwahisha kazini asubuhi
Juzi nilipokea ujumbe messenger kutoka kwa dada mmoja ambaye sikumfaham ila aliniomba namba ya simu akidai ana maongezi na mimi basi nikampatia namba nakupotezea
Asubuhi alinitafuta akiniuliza nipo wapi huku akitaka tuonane mida ya mchana kwa maongezi nae nilimwambia inabid nikufahamu kwanza vizuri before ya kukutana nawe lakini akanisihi nisiwe na shaka
Basi nilikutana nae maeneo aliyinielekeza na nilipofika niligundua hata yeye alikuwa hanijui kwani alinikaribisha kwa kusita kama hana uhakika na mimi, niliongea nae na akaweka wazi ya kuwa alikuwa amevutiwa na mimi kimapenzi akidai aliwahi niona nilipompelekea bidhaa moja ya wateja wangu ambaye ni rafiki ake.
Kwakwel sikukubaliana nae kwa pale nikamweleza wazi kuwa nina mke na ninampenda sana hivyo ni bora angetafuta mtu mwengne wa kuwa nae tuliachana japo hakuridhika na aliendeleza mawasiliano
Juzi alipiga simu na bahati mbaya simu ilikuwa kwa wife na namna nilivyosave ile namba ilimpa wasiwasi wife akaniletea simu nikaongea nae kawaida kama story sikutaka kumkazia ili wife asielewe chochote
Kumbe wife aliingiwa mashaka sana na aliichukua ile namba bila mimi kujua na alivyojaribu kuipiga akagundua ni ya mdada ambaye anamjua ni secretary wa ofisi yao na walikuwa close toka anaanza ajira pale ila hawakuwa na maelewano mazuri siku za hivi karibuni
Hivyo wife wangu akahoji imekuaje kuanza kuwasiliana nae na ni mahusiano gani yanayotuunganisha basi nikamwelezea wife ilivyokuwa akawa amechukia sana akasema atafanya kila namna huyu binti kumtimua kazini kwani ni wazi alifanya makusudi kwa kujua kwani walikuwa marafiki sana hapo awali
Nikamtafuta yule binti nikajaribu kumbana na kumweleza kuwa wife amechukua namba yake alishtuka sana na kusema nimsamehe kwan ni kweli alikuwa akijuana na mke wangu na ni boss wake lakini alitaka kumkomoa eti wife amekuwa mtu wa kuringa sana hapo ofisini akakiri na namba yangu alikuwa nayo before hajaniomba ila alizuga tu kupitia messenger ili isiwe rahisi kwangu kuelewa
Wife leo hakwenda kazini na alimpigia simu huyu dada zaidi ya mara 5 lakini hakupokea na hapa alipo kila nikijaribu kumshauri apotezee hili suala asimuharibie mtoto wa watu kazi ananiwakia anadai basi lengo letu ni moja
Huyu bint katuma meseji anajilaumu na ameingiwa na hofu na mimi nimeshndwa kumsaidia eti ananiomba nimwambie wife kuwa ni mimi niliemtafuta ili niokoe ajira yake mimi hapa nilipo sielewi wife toka jana hayupo sawa na amechukia hashauriki tena. Naomba mawazo yenu jamani namna ya kulimaliza hili soo bila huyu manzi kupoteza kazi na mimi ndoa yangu ibaki salama
Mkuu biashara zangu zimeyumba kidogo ndio maana akawa ana majukumu yote yeye lakini before hana ajira mambo yote nilikuwa namaliza mwenyeweKiongozi mkuu Gwele ni dhahiri sasa ngoma imekushinda, samahani kama nitakukwaza, kuanza kutetereka kwenye uchumi na kumpa mamlaka mama kuendesha familia ni kosa kubwa umefanya, ona sasa amepata nguvu ya ziada linapotokea tatizo kwako haambiliki, anajuwa fika kwa sasa yeye ndio starring wa mchezo . Mke mwema ni yule anaedhibiti hasira zake na hasa anaposhauriwa na mume kufanya hivyo. Sasa hapo una two alternatives chagua moja. 1. Mtafute rafiki yake/ndugu anaemuheshimu sana muite hapo kwako asemezane nae na wewe ukiwepo na ule kiapo kwa Mungu kwamba hamkufanya baya lolotebaina yenu na kwamba mke wako asamehe. 2. Tumia nguvu kama mwanaume kidogo weka mkwala, kwamba kama akifanya anayodhamiria na wewe utachukua hatua dhidi yake kwa anayoyafanya bila ya kutaja hatua gani na mambo gani. Yumkini na yeye ana mapungufu yake kwa vile anafanya kazi na anajichanganya na jinsia tofauti. Fanya hivyo uje leta mrejesho
Nashukuru mkuu kwa ushaur huuNdoa kwanza mkuu, huyo mdada atajibeba mwenyewe maana hakua na lengo jema na wewe, ushafikiria km alikua anakujua kabla na anajua wewe ni mme wa boss wake na ungemkubali kirahisi ukijua umependwa kumbe alkua na lengo la kukuharibia ndoa yako?
Kaa upande wa mkeo huyo dada achana nae, unavyozidi kumtetea wife ataamini kuna kitu kati yenu kweli, shauri yako
Ushauri huu ni mzuri mkuu nitajaribu kuufanyia kazi ili yeye abaki kazini na wife asinifikirie vibayaDawa ni kumleta mbele ya wife aje akiri huo mpango wake na aombe msamaha mbele yake akiri kosa lake baada ya hapo wife wako ndo atoe maamuzi.
Sidhani kama wife atapoteza uaminifu kwa hili kwani nilimkataa yule binti mapema tu
Hili suala ni gumu sana. Muache mke wako apambane nalo kwa jinsi anavyotaka.Wana jamvi nina mke wangu ambaye ni HR katika kampuni fulani hapa Dar na mimi ni mfanyabiashara japo mambo yangu yameyumba sana kwa sasa hivyo wife ambaye ndio amepata ajira mwaka huu anaboost sana mambo ya familia na next week alipanga tuvute usafiri ili kurahisisha shughuli zetu na pia kumuwahisha kazini asubuhi