Nashindwa kumsaidia

Gwele

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2016
Posts
2,773
Reaction score
3,527
Wana jamvi nina mke wangu ambaye ni HR katika kampuni fulani hapa Dar na mimi ni mfanyabiashara japo mambo yangu yameyumba sana kwa sasa hivyo wife ambaye ndio amepata ajira mwaka huu anaboost sana mambo ya familia na next week alipanga tuvute usafiri ili kurahisisha shughuli zetu na pia kumuwahisha kazini asubuhi

Juzi nilipokea ujumbe messenger kutoka kwa dada mmoja ambaye sikumfaham ila aliniomba namba ya simu akidai ana maongezi na mimi basi nikampatia namba nakupotezea

Asubuhi alinitafuta akiniuliza nipo wapi huku akitaka tuonane mida ya mchana kwa maongezi nae nilimwambia inabid nikufahamu kwanza vizuri before ya kukutana nawe lakini akanisihi nisiwe na shaka

Basi nilikutana nae maeneo aliyinielekeza na nilipofika niligundua hata yeye alikuwa hanijui kwani alinikaribisha kwa kusita kama hana uhakika na mimi, niliongea nae na akaweka wazi ya kuwa alikuwa amevutiwa na mimi kimapenzi akidai aliwahi niona nilipompelekea bidhaa moja ya wateja wangu ambaye ni rafiki ake.

Kwakwel sikukubaliana nae kwa pale nikamweleza wazi kuwa nina mke na ninampenda sana hivyo ni bora angetafuta mtu mwengne wa kuwa nae tuliachana japo hakuridhika na aliendeleza mawasiliano

Juzi alipiga simu na bahati mbaya simu ilikuwa kwa wife na namna nilivyosave ile namba ilimpa wasiwasi wife akaniletea simu nikaongea nae kawaida kama story sikutaka kumkazia ili wife asielewe chochote

Kumbe wife aliingiwa mashaka sana na aliichukua ile namba bila mimi kujua na alivyojaribu kuipiga akagundua ni ya mdada ambaye anamjua ni secretary wa ofisi yao na walikuwa close toka anaanza ajira pale ila hawakuwa na maelewano mazuri siku za hivi karibuni

Hivyo wife wangu akahoji imekuaje kuanza kuwasiliana nae na ni mahusiano gani yanayotuunganisha basi nikamwelezea wife ilivyokuwa akawa amechukia sana akasema atafanya kila namna huyu binti kumtimua kazini kwani ni wazi alifanya makusudi kwa kujua kwani walikuwa marafiki sana hapo awali

Nikamtafuta yule binti nikajaribu kumbana na kumweleza kuwa wife amechukua namba yake alishtuka sana na kusema nimsamehe kwan ni kweli alikuwa akijuana na mke wangu na ni boss wake lakini alitaka kumkomoa eti wife amekuwa mtu wa kuringa sana hapo ofisini akakiri na namba yangu alikuwa nayo before hajaniomba ila alizuga tu kupitia messenger ili isiwe rahisi kwangu kuelewa

Wife leo hakwenda kazini na alimpigia simu huyu dada zaidi ya mara 5 lakini hakupokea na hapa alipo kila nikijaribu kumshauri apotezee hili suala asimuharibie mtoto wa watu kazi ananiwakia anadai basi lengo letu ni moja

Huyu bint katuma meseji anajilaumu na ameingiwa na hofu na mimi nimeshndwa kumsaidia eti ananiomba nimwambie wife kuwa ni mimi niliemtafuta ili niokoe ajira yake mimi hapa nilipo sielewi wife toka jana hayupo sawa na amechukia hashauriki tena. Naomba mawazo yenu jamani namna ya kulimaliza hili soo bila huyu manzi kupoteza kazi na mimi ndoa yangu ibaki salama
 
Be the first to reply
 
Cha kufanya mtafute kama ni mzuri mzuri mtafune. Dawa ya wanawake ni wa kuwatafuna tu. Ukisha mtafuna ficha hio line waparangane wao kwa wao. Mtafute haraka nasema mtafute kisha mtafune
Mkuu katapoteza ajira haka kabinti hicho kinaniuma
 
Acha kutudhalilisha wanaume, hiv unamuoneaje huruma mtu alietaka kukuharibia ndoa yako kwa makusudi?Hujui kama mngeachana na mkeo pia huyu Dada msingedumu?Acha hizo mkuu open your mind budaa.
 
Cha kufanya mtafute kama ni mzuri mzuri mtafune. Dawa ya wanawake ni wa kuwatafuna tu. Ukisha mtafuna ficha hio line waparangane wao kwa wao. Mtafute haraka nasema mtafute kisha mtafune
Mwenzako unalelewa unataka afukuzwe hapo yenyewe mkewe ana mlia timing tu ajiandae kusaidiwa na wanaume wenzake
 
Tafuna Mzee baba Piga mbupu mpaka wanyooke asikutishe huyo
 
Acha kutudhalilisha wanaume, hiv unamuoneaje huruma mtu alietaka kukuharibia ndoa yako kwa makusudi?Hujui kama mngeachana na mkeo pia huyu Dada msingedumu?Acha hizo mkuu open your mind budaa.
Ni kweli mkuu huyu binti angeniharibia ndoa kama nisingekuwa makini
 
Acha kutudhalilisha wanaume, hiv unamuoneaje huruma mtu alietaka kukuharibia ndoa yako kwa makusudi?Hujui kama mngeachana na mkeo pia huyu Dada msingedumu?Acha hizo mkuu open your mind budaa.
Huyu ni mwanaume suruali hana akili kabisa mkewe kapata mzigo anamhurumia mchepuko, na hapo mkewe hamwamini
 
kausha tu acha wife afanye ajuavyo ajiridhishe..
 
Mna watoto????

Huenda wanakufanyia maigizo,huyo dada aliposema number yako alikua nayo toka awali ungemuuliza kwa kina aliipata vipi???

wife wako pia muulize kama aliwahi kuwa katika mazingira yaliyopelekea huyo dada kushika simu yake.

Mwisho mwache afukuzwe iwe funzo kwake na kwa wengine,kutofautiana ktk shughuri za kikazi anataka kuvunja ndoa unaweza kuta chanzo cha tatizo ni yeye.
 
Namba bila shaka aliiba kwa wife kwani walikuwa karibu sana hapo mwanzoni
 
Huyu ni mwanaume suruali hana akili kabisa mkewe kapata mzigo anamhurumia mchepuko, na hapo mkewe hamwamini
@cariha usiseme mchepuko sina mpango nae wowote huyu dada isipokuwa anatia huruma namna anavyoniomba kumsaidia lakini mimi pia sio mwanaume suruali napambana japo mambo yapo kushoto kidogo kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…