Nashindwa kulala.....msaada wa haraka unahitajika

Nashindwa kulala.....msaada wa haraka unahitajika

daviey69

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
2,234
Reaction score
873
Za Asubuhi wote.

Ni hivi mimi nimepangisha chumba maeneo flani hivi, na nyumba hiyo ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya familia kwahiyo ina sebule ambapo mlango mkubwa upo wa watu wote(wapangaji wanne ambao kati yetu wawili wanafamila zenye watoto na familia moja kati ya hizi zenye watoto alikodi chumba kimoja ila akaomba atumie na sebule of which hakuna aliyepinga) hupitia hapo, ki kawaida siku za kazi huwa nalala kuanzia saa mbili na nusu kwa ajili ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika na week end ndo naamsha popo tena si kidogo!

Tatizo linakuja pale ambapo wapangaji wenzangu haswa wenye familia, ikifika kuanzia saa moja watoto ndo wanakuwa kama ndo muda wao wakucheza au saa ingine ndo kupigana au kupigwa na wazazi wao baada ya kutokuoga ama kukataa kuoga!

Muda mwingine mama zao kwenye saa tatu au nne ndo wamemaliza kupika na kurudisha majiko na vitu walivyopika sebuleni, ghafula unasikia ngriiiiiiiiiiiiiii ngriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ngriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii wanatengeneza juice mda huo mara mwingine kaweka movie tena za kibongo(ambazo mara watu wanalia, mara wanacheka, mara mziki mkubwa usioendana na maudhui ya movie) kwa sauti ya juu mpaka mtu kama ulikuwa unasinzia unamka ghafla ukijua kuna watu wanagombana sebuleni!

OMBI: Jana baada ya kuchoshwa na hali hiyo nikatoka sebuleni TV zimewashwa mbili, familia moja inaangalia movie yenye watu wanaolia kila mda na kwa sauti ya juu upande mmoja wa sebule na famila nyingine inaangali channel five na huku wanatengeneza juice kwa zile mashine za brenda sijui grenda, nikachoka..... nikawaomba wapunguze sauti na nikarudi kulala lakini hawakupunguza mpaka baada ya kama dk 15 hivi!
Hali hii ikanipelekea kuwaza nipigishe shoti huku ndani kwangu cable zote za ukutani na taa zizimike? ila nikashindwa jinsi gani ntafanya zoezi hilo lisiwe na madhara sana kwa vyombo na liwe sustainable?

Nishaurini jinsi ya kufanya zoezi hilo ama otherwise....sio siri nakereka kinyama maana tatizo ni la kila siku!
 
daviey69 hio ndio rahisi ghali...natumaini nyumba ya kushare ni gharama nafuu kuliko kupanga nyumba nzima lakini gharama zake ndio hizo...tafuta nyumba ya peke yako hata chumba na sebule inayojitegemea.
 
Last edited by a moderator:
daviey69 hio ndio rahisi ghali...natumaini nyumba ya kushare ni gharama nafuu kuliko kupanga nyumba nzima lakini gharama zake ndio hizo...tafuta nyumba ya peke yako hata chumba na sebule inayojitegemea.
Thank man ila kwanini mtu ashindwe kujua jambo fulani linawakera wenzio haswa ukizingatia na mda?

Nimefikiria siku moja nirudi niko ganzi haswa na chupa nyingine mkononi huku naendelea kujidunga ili nizimike kabisa niweke porno movie tena kwa sauti ya juu...halafu nione kesho yake wataniambia nini!

Siwezi kuji-overbudget kisa watu wasio jitambua! saa ingine mambo ni mengi muhimu sana yenye kuhitaji financing!
 
Sasa naona unatafuta jela kama uvumilivu umekushinda hama.
 
Solution hapo ni kutafuta chumba chenye privacy unayohitaji na kuchapa lapa. Achana na mawazo ya kukorofisha umeme.

Lakini pia ni experience unapata maana siku si nyingi ukiwa na familia hayo ni mambo ya kawaida, tena siyo kelele tu ni kwamba dogo anazama chumbani bila hodi ( na wana haki ya kufanya hivyo kwasababu ni watoto na hawajapata ufahamu mkubwa wa kuainisha mambo). Hii ya kelele za watoto haijalishi kwamba ni uswahilini au kwingineko.
 
Hama uswazi bwana. Achana na shoti.
yaani nimecheka kama mwehu. Khaa
 
Hama uswazi bwana. Achana na shoti.
Yaani nimecheka kama mwehu. Khaa
Kukweli sio uswazi kivile ila ni ustarabu hakuna....mchana ni shwari na wapo na hawaendi mahali! Usiku tu ndio tatizo linaanza hapo! Nyumba nzima tupo wanne na ni ndani ya geti!
 
Anza kuwagegeda hao wanawake mmoja baada ya mwingine heshima itakuwepo.
 
Solution hapo ni kutafuta chumba chenye privacy unayohitaji na kuchapa lapa. Achana na mawazo ya kukorofisha umeme.

Lakini pia ni experience unapata maana siku si nyingi ukiwa na familia hayo ni mambo ya kawaida, tena siyo kelele tu ni kwamba dogo anazama chumbani bila hodi ( na wana haki ya kufanya hivyo kwasababu ni watoto na hawajapata ufahamu mkubwa wa kuainisha mambo). Hii ya kelele za watoto haijalishi kwamba ni uswahilini au kwingineko.
Madogo hawana shida kiivyo sana tatizo mama zao ndo kero zaidi kuliko madogo!

Hata hivyo wazo lako pia ntalifanyia kazi!
 
Back
Top Bottom