Uchaguzi 2020 Nashauri Serikali iahirishe Uchaguzi Mkuu mpaka 2030

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari Jf!

Baada ya kula chakula cha mchana nakushiba kuna wazo limenijia ,nikaona niishauri serikali japo serikali inawashauri wake sasa sidhani kama watapokea ushauri wangu.

Binafsi nlikuwa nawaza kwa sauti ila nikaona bora nitumie vidole alivyonipa Mungu kuandika mawazo yangu ili nitimize haki yangu ya kikatiba ya kutoa mawazo.

Mimi nimewaza mbali sana sitaki kusema ni umbali wa kilometa ngapi ,ila naishauri serikali pesa iliyopanga kuwekeza kwny uchaguzi iende azina na uchaguzi uhalishwe kwa kipindi kisichojulikana mpaka hapo 2030 ndio itangaze tarehe rasmi ya uchaguzi.

Kuna kila dalili kwamba mpaka sasa kama uchaguzi utafanyika 2020 Magufuli atapita kwa 100% ebu ili tulitazame jamani ,hapa kuna aja gani ya kuendelea na uchaguzi?

Dunia sasa hivi iko kwenye tishio kubwa la Corona na sasa ugonjwa huu ushaingia Afrika ,hivyo hizi hela kama tutazichezea kwny uchaguzi ambao mshindi anajulikana badae tutakuja kulia kilio cha mbwa koko.

Tumeona wengi wakiunga mkono juhudi za mheshimiwa rais that mean upinzani umeshakufa mpaka ss waliobaki wanatupotezea mda tu kwa kweli kama vipo vyama vyao vifutiliwe mbali tubaki na chama kimoja mpaka 2030 ili tujenge kwanza uchumi wa nchi maana uchumi wa dunia unatabiliwa mda wowote utashuka kwa kasi kutokana na Corona Virus.

Wewe mwenzangu unasemaje?
 
Ni hoja fikirishi, yaani hata kama mtaamua kufanya uchaguzi kwa Tume hii na mazingira haya ya kisiasa unapata nini zaidi ya kujichosha, majeruhi na vifo vingi.

Ni changamoto kwa wapinzani na wapigania demokrasia nchini kuliona mambo hili.

Kama tume haipatikani, basi yaishe aliyeko aendelee hadi hapo tutakapopata akili na uthubutu wa kudai tume huru...tuliojoe taifa kwa upotevu wa fedha nyingi kwa uchaguzi feki..ndiyo mwacheni aliyeko madarakani atawale.
 
Habari Jf!

Baada ya kula chakula cha mchana nakushiba kuna wazo limenijia ,nikaona niishauri serikali japo serikali inawashauri wake sasa sidhani kama watapokea ushauri wangu.

Binafsi nlikuwa nawaza kwa sauti ila nikaona bora nitumie vidole alivyonipa Mungu kuandika mawazo yangu ili nitimize haki yangu ya kikatiba ya kutoa mawazo.

Mimi nimewaza mbali sana sitaki kusema ni umbali wa kilometa ngapi ,ila naishauri serikali pesa iliyopanga kuwekeza kwny uchaguzi iende azina na uchaguzi uhalishwe kwa kipindi kisichojulikana mpaka hapo 2030 ndio itangaze tarehe rasmi ya uchaguzi.

Kuna kila dalili kwamba mpaka sasa kama uchaguzi utafanyika 2020 Magufuli atapita kwa 100% ebu ili tulitazame jamani ,hapa kuna aja gani ya kuendelea na uchaguzi?

Dunia sasa hivi iko kwenye tishio kubwa la Corona na sasa ugonjwa huu ushaingia Afrika ,hivyo hizi hela kama tutazichezea kwny uchaguzi ambao mshindi anajulikana badae tutakuja kulia kilio cha mbwa koko.

Tumeona wengi wakiunga mkono juhudi za mheshimiwa rais that mean upinzani umeshakufa mpaka ss waliobaki wanatupotezea mda tu kwa kweli kama vipo vyama vyao vifutiliwe mbali tubaki na chama kimoja mpaka 2030 ili tujenge kwanza uchumi wa nchi maana uchumi wa dunia unatabiliwa mda wowote utashuka kwa kasi kutokana na Corona Virus.

Wewe mwenzangu unasemaje?
Uchaguzi unawapa wananchi heshima kwa watawala. Ona serikali inavyohangaika kutangaza kila kitu inachofanya na kunyamazisha upinzani. Yote haya ni kwasababu wanajua wananchi waliomuua nini 2015.
 
Ukiwa na njaa hauwezi pata mawazo mazuri boss!

Sio kwamba Magufuli ana uwezo wa kushinda kwa 100%, ni kwamba Magufuli anatamani ashinde kwa 100%, hivyo anatumia nafasi yake ya kimadaraka kuzuia wapinzani wake kwa matumizi mabaya ya madaraka, na kwakuwa hawezi ushindani wa kisiasa, anatengeneza propaganda za kuuhadaa umma kuwa anakubalika sana hivyo kusiwe na uchaguzi, kwa sababu anajua fika hana uwezo wa kupata asilimia 50 ya kura kihalali.
 
Back
Top Bottom