Nashauri Bunge lipunguziwe bajeti

Fisadidagaa

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
962
235
Habari wakuu,
kutokana na kile kilichoitwa kubana matumizi kwa Bunge la jamuhuri ya Muungano kiasi cha zaidi ya bilioni 6,na fedha hizo kukabidhiwa muheshimiwa Rais kupitia kwa naibu spika wa Bunge,na hivyo kupangiwa kazi nyingine {wamesema madawati},ninalo wazo.
Inaonekana bajeti waliyopata na walizowahi kupata huko nyuma ni kubwa na inawezekana kuwa huwa kuna wajanja wachache huwa wanatia mfukoni,maana hata Mh.Rais mwenyewe amekiri kuwa walikuwa {Bunge}na uwezo wa kuziandikia matumizi hata yasiyokuwepo,wakazitumia na hakuna ambaye angewahiji.
Au la tuamini ni sifa tu za kuonekana mnabana matumizi {Mzuka wa Magufuli},kumbe ni danganya toto,hivyo kwa kuanzia bajeti ya mwaka huu wa fedha zipunguzwe bilioni 6 nakama ikiwezekana zaidi ya hizo,ili zipangiwe kazi kwenye bajeti moja kwa moja.
Asante.
 
Sawa mkuu
 
Mkuu,
Ingekuwa ni vyema ukaweka na Data,
Sasa budget kiasi gani na upunguzwe kwa kiasi gani.
Mkuu,
Bajeti ya bunge kwa mwaka huu bado haijatoka,ila ya mwaka jana ambayo fedha walishapata wamedai wamebana matumizi hivyo zaidi ya bilioni 6 wamemkabidhi rais,hivyo kwa kuanzia nimeshauri waanze na kiasi hicho kupunguza katika bajeti ijayo,au la wapewe bajeti kama ya mwaka huu wa fedha unaomalizika maana zinabaki,na hiyo wamedai ni kwa kuanzia tuu wanaweza kubana zaidi miezi inayofuata.
 
Binge ni mhimili kama ilivyo serikali na Mahakama. Anza kuondoa ma V8 wanayotembelea kina Mwigulu na Likwelile, wape Chaser, Ondoa V8 za majaji wape Cresta then kapunguze bajeti ya Bunge
 
Naibu spika ameeleza bayana kuwa safari za nje na mafunzo ya nje yamepungua, posho za baadhi ya vikao zimepungua, wamebana pia matumizi ya utilities. Hapo alitakiwa apongezwe kwa vile wameendana na mabadiliko ya serikali mpya. Sasa tuwashangae ambao hawatarudisha

Ndio maana namlaani sana Zitto Kabwe kwa kauli aliyoitoa juzi baada ya muelekeo wa bajeti mpya kutoka akaanza kulia lia kuwa baadhi ya mashirika yamepunguziwa bajeti. Kumbe naye hajabadilika, ni jipu, bajeti ya JPM ijayo imekata matumizi yote ya hovyo yaliyokuwa kwa Kikwete so ni dhahiri hata bajeti ya bunge itapungua
 
hiyo hela imepatikana kwa miezi sita sas mwaka una miezi kumi na mbili , nashauri bunge lipunguziwe bilion 12
ili kuweza kubana matumizi
 
Binge ni mhimili kama ilivyo serikali na Mahakama. Anza kuondoa ma V8 wanayotembelea kina Mwigulu na Likwelile, wape Chaser, Ondoa V8 za majaji wape Cresta then kapunguze bajeti ya Bunge
Bila kusahau BMWs na Benzs za Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi n.k. Hili la kubana matumizi liwe kwa viongozi waandamizi wote. Siyo baadhi tubane matumizi, halafu wengine waendelee na matanuzi.
Waendeshwe kwenye Rav4 ama Suzuki Vitara. Na pia uanze utaratibu wa viongozi kujiendesha wenyewe (isipokuwa Rais, Makamu na Waziri Mkuu), na kutumia mfumo wa government pool, ambapo kiongozi husika atakodisha gari na kulitumia panapouhitaji tu.
 
Nadhani bajeti ya maendeleo ya mahakama ingeongezwa, tumeshuhudia siku hizi mahakama haikai na kesi muda mrefu baada ya kupewa fungu mahakama kuu na za rufani zipo kazini muda wote hakuna kuchelewesha kesi, kwa kupewa bajeti kubwa ya mahakama zitajengwa mahakama nyingi za mwanzo na wilaya ambazo zina mzigo mkubwa wa kesi na uhaba wa mahakimu, mengineyo ulioandika pokea like yangu
 
Binge ni mhimili kama ilivyo serikali na Mahakama. Anza kuondoa ma V8 wanayotembelea kina Mwigulu na Likwelile, wape Chaser, Ondoa V8 za majaji wape Cresta then kapunguze bajeti ya Bunge
Ma V8 yameshanunuliwa maana yake bajeti ilishapita,naongelea haya yanayoendelea.
 
Naibu spika ameeleza bayana kuwa safari za nje na mafunzo ya nje yamepungua, posho za baadhi ya vikao zimepungua, wamebana pia matumizi ya utilities. Hapo alitakiwa apongezwe kwa vile wameendana na mabadiliko ya serikali mpya. Sasa tuwashangae ambao hawatarudisha

Ndio maana namlaani sana Zitto Kabwe kwa kauli aliyoitoa juzi baada ya muelekeo wa bajeti mpya kutoka akaanza kulia lia kuwa baadhi ya mashirika yamepunguziwa bajeti. Kumbe naye hajabadilika, ni jipu, bajeti ya JPM ijayo imekata matumizi yote ya hovyo yaliyokuwa kwa Kikwete so ni dhahiri hata bajeti ya bunge itapungua
Hapo kwenye nywkundu kama kweli basi wapo sawa na mawazo yangu.
 
Back
Top Bottom